Pata taarifa kuu
PAKISTANI-TALIBAN-Usalama

Zaidi ya watu 140 wauawa Peshawar

Kundi la wapiganaji wa Taliban wakiwa na zana nzito nzito wameendesha shambulio mapema Jumanne Desemba 16 asubuhi katika shule ya watoto wa askari katika mji wa Peshawar kaskazini magharibi mwa Pakistan.

Wanawake hawa wakilia baada ya kupata taarifa kuwa watoto zao wameuawa katika shambulio lililoendeshwa na wapiganaji wa Taliban katika shule la watoto wa askari katika mji wa Peshawar, nchni Pakistan.
Wanawake hawa wakilia baada ya kupata taarifa kuwa watoto zao wameuawa katika shambulio lililoendeshwa na wapiganaji wa Taliban katika shule la watoto wa askari katika mji wa Peshawar, nchni Pakistan. REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na idadi iliyotolewa na viongozi, shambulio hilo limegharimu maisha ya zaidi ya watu 140, wengi wao wakiwa ni wanafunzi, na wengine wengi wamejeruhiwa.

Polisi imetangaza kuwa imewaua wauaji wote ambao wamekua wameshambulia shule hilo. Waziri mkuu Nawaz Sharif ameyaita mauwaji hayo kuwa ni janga la kitafa.

Jeshi la Pakistan limetangaza kuwa limerejesha hali ya utulivu katika mji wa Peshawar. Operesheni ya jeshi imetamatika baada ya kumuua mshambuliaji wa sita ambaye alikua wa mwisho. Operesheni hiyo imedumu saa 7. Hata hivyo operesheni hiyo imecheleweshwa kutokana na milipuko iliyokua ikisikika katika majengo ya shule hilo, afisa mmoja wa ngazi ya juu jeshini ameelezea kwenye akaunti yake ya Twitter.

Kundi la TTP ( TTP, le Tehreek-e-Taliban Pakistan), limekiri kuendesha shambulio hilo. Msemaji wa kundi hilo, amebaini kwamba shambulio hilo ni ulipizaji kisase kwa operesheni inayoendeshwa na jeshi katika ngome za kundi la Taliban katika eneo linalokabiliwa na mizozo ya kikabila la Waziristan ya Kaskazini, na amri ilitolewa ya kuwapiga risasi watu wa kubwa, baada ya kuwatenganisha na watoto.

Hili ni shambulio la pili baada ya miezi ya hivi karibuni kutokea shambulio jingine lililosababisha maafa makubwa nchini Pakistan, jeshi limekua likilengwa na mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.