Pata taarifa kuu

Korea Kaskazini yarusha kombora jipya la balistiki kuelekea Bahari ya Japan

Korea Kaskazini imerusha kombora lisilojulikana katika bahari karibu na pwani ya mashariki ya Korea Kusini, jeshi la Seoul limesema leo Jumatatu. Hili ni jaribio la hivi punde zaidi katika mfululizo wa majaribio yaliyofanywa na Pyongyang mwaka huu.

"Korea Kaskazini imerusha kombora lisilojulikana katika Bahari ya Mashariki" pia inaitwa Bahari ya Japan, makao makuu ya majeshi ya Korea Kusini imetangaza, baada ya Wizara ya Ulinzi ya Japan pia kuripoti "uwezekano wa kurushwakwa kombora la balestiki" uliofanywa na Pyongyang.
"Korea Kaskazini imerusha kombora lisilojulikana katika Bahari ya Mashariki" pia inaitwa Bahari ya Japan, makao makuu ya majeshi ya Korea Kusini imetangaza, baada ya Wizara ya Ulinzi ya Japan pia kuripoti "uwezekano wa kurushwakwa kombora la balestiki" uliofanywa na Pyongyang. via REUTERS - KCNA
Matangazo ya kibiashara

Korea Kaskazini imerusha kombora la balestiki siku ya Jumatatu Aprili 22 kuelekea baharini katika pwani yake ya mashariki, jeshi la Korea Kusini limetangaza.

"Korea Kaskazini imerusha kombora lisilojulikana katika Bahari ya Mashariki" pia inaitwa Bahari ya Japan, makao makuu ya majeshi ya Korea Kusini imetangaza, baada ya Wizara ya Ulinzi ya Japan pia kuripoti "uwezekano wa kurushwakwa kombora la balestiki" uliofanywa na Pyongyang.

Hapo awali, Wizara ya Ulinzi ya Japan pia iliripoti "uwezekano wa kurushwa kwa kombora la balestiki" na Pyongyang, katika ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Walinzi wa Pwani ya Japan, wakinukuu Wizara ya Ulinzi, wamesema muda mfupi baada ya kuwa kombora hilo lilionekana kuwa tayari limeanguka baharini lilianguka nje ya eneo la kipekee la kiuchumi la Japan (EEZ), kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Japan, ikiwa ni pamoja na shirika la utangazaji la NHK, likinukuu vyanzo visivyojulikana vya serikali.

Kulingana na tovuti ya wataalamu ya NK News, iliyoko Seoul, "ufupi wa safari hiyo, labda chini ya dakika kumi, unaonyesha kuwa uzinduzi ulihusisha kombora la masafa mafupi (SRBM) au mfumo wa roketi wa MLRS wa 600 mm".

Pyongyang inakabiliwa na msururu wa vikwazo na hata hivyo imeendelea kuendeleza mipango yake ya nyuklia na silaha. Hivi karibuni Korea Kaskazini imeimarisha uhusiano na Urusi, mshirika wake wa jadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.