Pata taarifa kuu
UHALIFU-USALAMA

Shambulio la bomu la kujitoa mhanga nchini Pakistani: Wajapani wauawa wakidhaniwa ni Wachina

Huko Karachi, kusini mwa Pakistan, Wajapani watano walinusurika shambulio la kujitoa mhanga kwenye gari ambalo liliwbebea siku ya Ijumaa Aprili 19. Mmoja wao alijeruhiwa kidogo. Washambuliaji wawili waliuawa. Wafanyakazi watano wa kampuni ya Japani walikuwa wakielekea katika eneo la viwanda la Karachi. Watu wa Japani huwa hawaengwi sana na mashambulizi ya makundi yenye itikadi kali nchini Pakistan. Huko Tokyo, ripoti za vyombo vya habari zinaonyesha kuwa huenda walidhaniwa kuwa Wachina.

Baada ya shambulio lingine la kujitoa mhanga huko Karachi, Pakistani, Aprili 19, 2024.
Baada ya shambulio lingine la kujitoa mhanga huko Karachi, Pakistani, Aprili 19, 2024. REUTERS - Akhtar Soomro
Matangazo ya kibiashara

Na mwanahabari wetu mjini Tokyo, Frédéric Charles

Nchini Pakistan, makundi yenye itikadi kali yana chuki kubwa dhidi ya miradi ya viwanda inayofadhiliwa na China. Mashambulizi yao mengi yanalenga raia wa China.

Kulingana na Nikkei, Gazeti la biashara nchini Japani, Wajapani watano waliokuwa wakisafiri hadi eneo la bandari la Karachi wakiwa kwenye gari la kivita wanaweza kuwa walidhaniwa kuwa ni raia wa China. Polisi wa Pakistani pia wanataja uwezekano kama huo.

"Japani haijawahi kuwa kwenye rada ya magaidi nchini Pakistan"

Shambulio hili litakuwa la kwanza dhidi ya wafanyakazi wa kampuni ya Japani nchini Pakistan. "Wajapani wanaofanya kazi Pakistani tayari walikuwa na hofu kwamba wanamgambo wa Pakistani wanaweza kuwadhania kuwa Wachina kwa sababu ya sura yao ya kimwili," mchambuzi aliyebobea katika masuala ya wanamgambo nchini Pakistan ameliambia Gazeti la Nikkei. Kwa Kuram Iqbal, mtaalam wa kukabiliana na ugaidi, anasema shambulio hili ni kisa cha utambulisho usio sahihi. "Japani haijawahi kuwa kwenye rada ya magaidi nchini Pakistan. "

Uwepo wa uchumi wa Japani nchini Pakistan ni mdogo ikilinganishwa na ule wa China. Miradi inayofadhiliwa na China inatajwa kutoleta manufaa yoyote kwa wakazi wa eneo hilo, huku kazi nyingi zikienda kwa wafanyakazi wa China.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.