Pata taarifa kuu

Xi Jinping: Beijing na Washington lazima ziwe 'washirika, sio mahasimu'

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken, ambaye amemaliza ziara yake nchini China, amekutana na viongozi wa China akiwemo Xi Jinping siku ya Ijumaa. Rais wa China amekaribisha maendeleo yaliyopatikana kati ya nchi hizo mbili, ingawa matatizo mengi bado yanahitaji kutatuliwa, amesema.

Le secrétaire d'État américain, Antony Blinken, rencontre le président chinois, Xi Jinping, au Grand Palais du Peuple. Pékin, Chine, le 26 avril 2024.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken akutana na rais wa China Xi Jinping katika ukumbi wa Great Hall of the People, Beijing, China, Aprili 26, 2024. © via REUTERS - Mark Schiefelbein
Matangazo ya kibiashara

Dunia ni kubwa na inatosha kwa pande mbili. China na Marekani lazima ziwe "washirika, si mahasimu," Xi Jinping amesema, lakini ili hili lifanyike, Marekani lazima iwe na maono chanya kuhusu maendeleo ya China.

Hoja hii ya utawala wa Marekani kutaka kuzuia kuinuka kwa uchumi wa pili kwa ukubwa duniani si mpya. Ilijadiliwa pia wakati wa saa tano na nusu za majadiliano ya "kina na ya kujenga" - kulingana na upande wa Marekanni - kati ya Antony Blinken na mwenzake Wang Yi asubuhi hiyo hiyo. Waziri wa Mambo ya Nje wa China amekumbusha mstari mwekundu ambao Taiwan inafanya kwa Uchina.

Katika mkutano na waandishi wa habari mwishoni mwa siku katika Ubalozi wa Marekani, Antony Blinken alisema ameonya mamlaka ya China dhidi ya mazoezi hatari karibu na Ufilipino.

Makubaliano ya pointi tano yalichapishwa na vyombo vya habari vya serikali: pande hizo mbili zinakubali kudumisha mazungumzo katika ngazi zote na kuendelea na jitihada zao za kuimarisha mahusiano yao. Pia wanatangaza kufanyika kwa mazungumzo yanayokuja kati ya China na Marekani juu ya akili ya bandia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.