Pata taarifa kuu

Putin kutawazwa kama rais wa Urusi kwa muhula wa tano

Vladimir Putin anatarajiwa kuapishwa leo Jumanne kama rais wa Urusi kwa muhula wa tano, ambapo yuko mamlakani kwa muda mrefu bila kupingwa licha ya upinzani uliokandamizwa, katikati ya msukumo wa wanajeshi wa Urusi kwenye uwanja wa vita nchini Ukraine.

Rais wa Urusi pia alishinda jaribio la uasi mwaka jana lililoendeshwa na kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo wa Wagner, Yevgeni Prigozhin, ambaye alifariki katika ajali ya ndege yake.
Rais wa Urusi pia alishinda jaribio la uasi mwaka jana lililoendeshwa na kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo wa Wagner, Yevgeni Prigozhin, ambaye alifariki katika ajali ya ndege yake. AP
Matangazo ya kibiashara

Takriban miezi miwili baada ya uchaguzi wa marudio ulioonyeshwa na Kremlin kama ushindi, kwa kukosekana kwa mgombea mpinzani, mkuu wa serikali wa Urusi, mwenye umri wa miaka 71 na aliye madarakani kwa karibu robo ya karne, atahudumu angalau hadi mwaka 2030. 

Mnamo mwaka 2020, alibadilisha Katiba ili kuweza kuhudumu mihula miwili ya ziada ya miaka sita, hadi mwaka 2036, mwaka ambao atakauwa ametimiza umri wa miaka 84.

Chini ya usimamizi wa Kremlin na mbele ya wasomi wa kisiasa wa nchi na wawakilishi wa kigeni, pamoja na balozi wa Ufaransa, uzinduzi sherehe za kuapishwa zitaanza saa 6:00 mchana kwa saa za ndani na kudumu karibu saa moja, kulingana na vyombo vya habari vya Urusi.

Nchi nyingine za Ulaya, kama vile Poland, Ujerumani na Jamhuri ya Czech, zimebaini kwamba hazitatuma wawakilishi, kuashiria upinzani wao kwa sera za Kremlin.

Wakati wa hafla hiyo, Vladimir Putin atakula kiapo kabla ya kutoa hotuba fupi kwa Taifa.

Hotuba ambayo inakuja mwaka huu siku mbili kabla ya kumbukumbu ya ushindi wa Soviet wa Mei 9 dhidi ya Ujerumani ya Kinazi, sherehe ambayo ni nguzo ya sera ya nguvu ya Vladimir Putin, ambaye anadai kupigana na "Neo-Nazi.

- "Udanganyifu wa demokrasia" -

Kuapishwa huko kunaambatana na hali nzuri zaidi mbele ya jeshi la Urusi, ambalo lilipata shida za kufedhehesha katika msimu wa joto na wa baridi wa mwaka 2022, wakati wa miezi ya kwanza ya shambulio lake kubwa dhidi ya Kyiv.

Katika wiki za hivi karibuni, mashambulio ya Urusi mashariki mwa Ukraine yameongezeka kwa kasi na kuwezesha ushindi wa taratibu wa maeneo kadhaa, haswa katika eneo la mji muhimu wa Avdiïvka, uliotekwa katikati ya mwezi wa Februari.

Kinyume chake, wanajeshi wa Kyiv wanakosa risasi na vifa vingine vya kijeshi baada ya shambulio lao ambalo halikufanikiwa katika msimu wa joto wa 2023. Wanangojea kuwasili kwa msaada mpya wa Marekani, wakati tasnia ya ulinzi ya Urusi inaendelea kikamilifu.

Katika jiji la Moscow, vizuizi vingi vimewekwa kando ya njia kuu katika maandalizi ya kuapishwa kwa rais Putin na gwaride la kijeshi mnamo Mei 9.

Sherehe ambayo Ukraine ilishutumu kama udanganyifu wa demokrasia.

Siku ya Jumatatu diplomasia ya Ukraine ilibaini kwamba ilikusudiwa kutoa "udanganyifu wa uhalali" kwa kusalia madarakani kwa Bw. Putin, ambaye, kulingana na Kyiv, alibadilisha Urusi kuta "taifa chokozi" na utawala uliopo kuwa wa "kiimla".

- Ukandamizaji -

Katikati ya mwezi wa Machi, kufuatia kura aliyoshinda rasmi kwa zaidi ya 87% ya kura zilizopigwa, Vladimir Putin alichora picha ya Urusi "iliyoungana" nyuma yake na jeshi lake.

Wamagharibi, wakiongozwa na Washington, kwa upande wao walipinga uchagzi wa kulazimishwa, wiki chache baada ya kifo cha mpinzani mkuu wa Urusi, Alexeï Navalny alifariki akiwa gerezani katika mazingira ya kutatanisha, mnamo Februari 16.

Wanachama wakuu wa upinzani wa Urusi sasa wako uhamishoni au gerezani, kama vile mamia ya watu wa kawaida ambao wametoa maoni yao ya kupinga hujuma ya Moscow dhidi ya jirani yake Ukraine.

Kitanzi pia kimeimarishwa dhidi ya jamii ya walio wachache kijinsia, ambao tayari walilengwa na ukandamizaji mkali na ambao hulipa gharama za kukuza "maadili ya jadi" yanayotetewa na Bw. Putin mbele ya Magharibi inayochukuliwa kuwa potovu.

Rais wa Urusi pia alishinda jaribio la uasi mwaka jana na kiongozi wa zamani wa kundi la wanamgambo wa Wagner, Yevgeni Prigozhin, ambaye alifariki katika ajali ya ndege yake.

Mkuu wa Ikulu ya Kremlin hata hivyo anakabiliwa na changamoto kadhaa, hasa za kiuchumi, huku matokeo ya mzozo wa Ukraine, ambao ni hatari sana, bado yanaonekana kutokuwa na uhakika.

Mfumuko wa bei, unaoendeshwa haswa na mlipuko wa bajeti ya shirikisho, unaohusishwa na matumizi ya kijeshi, bado unaendelea na unatia wasiwasi raia, ambao uwezo wao wa kununua tayari umezimwa na athari za vikwazo vya Magharibi.

Na uchumi wa Urusi, unaotegemea sana mapato ya hydrocarbon, lazima pia ujadili mabadiliko, yaliyodaiwa na Vladimir Putin, kuelekea Asia, hata ikiwa miundombinu muhimu, ya gharama kubwa na inayotumia wakati mrefu kwa kujenga, bado haipo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.