Pata taarifa kuu

Mkuu wa idara ya ujasusi ya Israeli Aharon Haliva ametangaza kujiuzulu

Mkuu wa idara ya ujasusi katika jeshi la Israeli ametangaza kujiuzulu kuhusiana na kile ambacho kimetajwa kama kufeli kuzuia shambulio la Hamas la tarehe saba ya mwezi Oktoba mwaka uliopita.

Meja Jenerali Aharon Haliva amekuwa afisa wa kwanza wa ngazi ya juu kuachia nafasi yake
Meja Jenerali Aharon Haliva amekuwa afisa wa kwanza wa ngazi ya juu kuachia nafasi yake © Israeli Defence Forces Spokesperson's Unit
Matangazo ya kibiashara

Meja Jenerali Aharon Haliva amekuwa afisa wa kwanza wa ngazi ya juu kuachia nafasi yake kutokana na shambulio hilo ambalo limetajwa kuwa baya zaidi katika historia ya Israeli.

Wachambuzi wa masuala ya kiusalama wanasema kuwa hatua hii huenda ikatoa nafasi kwa maofisa wengine wakuu katika idara ya usalama kufanya hivyo kutokana na kilichotokea wakati wa shambulio hilo.

Israeli inasema inawaka wapiganaji wa Hamas katika ukanda wa Gaza waliohusika na shambulio dhidi yake
Israeli inasema inawaka wapiganaji wa Hamas katika ukanda wa Gaza waliohusika na shambulio dhidi yake via REUTERS - Handout .

Zaidi ya watu 1,200 raia wa Israeli waliripotiwa kuuawa katika shambulio hilo la wapiganaji wa Hamas ambapo pia watu wengine 250 walichukuliwa mateka.

Israeli ilichukua hatua ya kujibu shambulio dhidi ya wapiganaji wa Hamas katika ukanda wa Gaza, makabiliano ambayo kwa sasa yameingia katika mwezi wa saba.

Israeli imeapa kuendelea na vita vyake dhidi ya Hamas licha ya wito wa kimataifa wa kutaka kusitishwa wa mapigano
Israeli imeapa kuendelea na vita vyake dhidi ya Hamas licha ya wito wa kimataifa wa kutaka kusitishwa wa mapigano REUTERS - RONEN ZVULUN

Vita vya Israeli na Hamas vimeonekana kuchukua mkondo mwengine, nchi ya Iran mshirika wa Palestine ikionekana kuwa katika mzozo na Israeli, wapiganaji wa Hezbollah kutoka Lebanon nao pia wakionekana kuingia kwenye mzozo huo.

Iran ilirusha makombora kuelekea Israeli ikidai kuwa inalipiza kisasa shambulio dhidi ya ubalozi wake mdogo mjini Damascus.

Soma piaIran kujibu vikali iwapo Israeli italipiza kisasi shambulio la wikendi iliopita

Haliva, pamoja na wanajeshi wengine na wakuu wa usalama walitarajiwa kujiuzulu kutokana na tuhuma kuwa walishindwa katika wajibu wao wa kuzuia shambulio hilo na tarehe saba mwezi Oktoba.

Vita vilivyotokana na shambulio hilo vimesababisha vifo vya zaidi ya raia elfu 34 wa Palestina katika Ukanda wa Gaza kwa mujibu wa wizara ya afya inayoongozwa na Hamas.

RFI- Kiswahili/AP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.