Pata taarifa kuu
Sudani-mapigano

Milio ya risase yasikika katika mji mkuu wa Sudani Kusini Juba.

Milio ya risase imesikika leo asubuhi katika mji mkuu wa Sudani Kusini wa Juba katika eneo la kituo cha jeshi. Mashahidi wanasema milio hiyo ya risase inatokea katika kituo cha jeshi cha Giyada kilichopo karibu na chuo kikuu cha na kudumu kwa muda saa mbili.

Matangazo ya kibiashara

Habari zinazo kinzana zimekuwa zikizagaa kwamba wanajeshi wanadhihirisha hasira yao kwa kutopewa viinuwa mgogo, huku wengine wakisema ni kundi la wanajesi wengine wanaoasi jeshi la serikali wakati huu nchi hiyo ikiwa katika mapigano tangu katikati mwa mwezi Desemba mwaka jana.

Kwa mujibu wa kituo huru cha habari cha Tamazuj jijini hapo, inahofiwa kuwa huenda majibizano hayo ya risase yamesababisha vifo vya watu licha ya kwamba ni vigumu kujuwa kinachoendelea. Mawasiliano ya msemaji wa Jeshi hayakufua dafu baada ya sim zake kutopatikana.

Ubalozi wa Marekani jijini Juba umewataka raia wa Marekani ambao bado wapo jijini Juba kutotembea usiku.

Sudani Kusini iliingia katika mzozo tangu Desemba 15 mwaka jana, ambapo mapiganao yanashuhudiwa kati ya wanajeshi wa serikali na waasi tiifu kwa makam wa kwanza wa zamani wa serikali Riek Mashar.

Mapigano hayo yalianzia mjini Juba kabla ya kutanda katika miji mingine nchini humo. Maelfu wa watu wanaripotiwa kupoteza maisha huku takriban watu laki tisa wakiyatoroka makwao.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.