Pata taarifa kuu
GUINEA

Virusi vya Ebola vyabainika kuwa chanzo cha homa na vifo nchini Guinea

Virusi vya Ebola vimetajwa kuwa chanzo cha kuibuka kwa ugonjwa wa homa inayoambatana na kuvuja damu, kusini mwa nchi ya Guinea, huku idadi ya vifo ikifikia watu 34. 

Virusi vya ebola
Virusi vya ebola CDC/ Cynthia Goldsmith
Matangazo ya kibiashara

Wataalam nchini humo wameshindwa kubaini ugonjwa huo unao ambukiza kwa kasi sana, ambao dalili zake ni kuharisha, kutapika na kutokwa na damu bila kukoma.

Wataalamu hao walifanya uangalizi wa wiki sita zilizopita bila mafanikio,lakini wanasayansi katika mji wa Lyon nchini Ufaransa wamehibitisha kuwa ugonjwa huo ni Ebola,

Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Watu wapatao 1,850 wamegundulika kuwa na ugonjwa huo tangu kugundulika kwa virusi vya ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo miaka 38 iliyopita na tayari watu 1200 wamepoteza maisha.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.