Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-UN-Ukimbizi

UN inatiwa hofu na hali ya raia wa Sudan Kusini walioko ukimbizini

Zaidi ya wakimbizi elfu moja toka nchi ya Sudan Kusini wanaingia nchini Ethiopia kila siku, huku wengi wao wakikabiliwa na hali mbaya na wako hatarini kupoteza maisha, na hii ni kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa UN.

Wakimbizi wa ndani kutoka Sudani Kusini  wakipewa hifadhi katika kambi ilyojengwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Khor Abeche.
Wakimbizi wa ndani kutoka Sudani Kusini wakipewa hifadhi katika kambi ilyojengwa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini Khor Abeche. REUTERS/Albert Gonzalez Farran
Matangazo ya kibiashara

Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake linaloshughulikia wakimbizi duniani UNHCR, unasema kuwa karibu asilimia 95 ya wakimbizi wanaoingia nchini humo wengi ni wanawake na watoto na kuongeza kuwa wengi walikuwa wakitumikishwa kwenye makundi ya wapiganaji nchini Sudan Kusini.

UNHCR inasema kuwa iwapo raia hao hawatapata msaada wa haraka, hali itakuwa mbaya zaidi na pengine kushuhudia vifo wakati huu nchi hiyo ikiwa inahifadhi wakimbizi zaidi ya elfu 95 wa Sudan Kusini.

Zaidi ya raia laki mbili wa Sudan Kusini wameomba hifadhi nchini Sudan, Uganda na Kenya wakati watu laki 8 hawana makaazi ya kudumu ndani ya Sudan Kusini yenyewe.

Machafuko nchini Sudan Kusini yamesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine zaidi ya 1.000.0000 wameyahama makaazi yao, laki 8 wakiwa ni wakimbizi wa ndani na wengine laki 3 wamekimbilia nje ya nchi.

Tangu machafuko kutokea 15 desemba mwaka 2013, raia wa Sudan Kusini 61.000 wamekimbilia Sudan, 97.000 wamekimbilia nchini Rwanda, 95.700 wamekimbilia nchini Ethiopia na 33.400 wanapewa hifadhi nchini Kenya, wakihofia usalama wao na njaa inayolikabili taifa hilo changa.

Wakimbizi 86.000 kutoka Sudan Kusini wamepewa hifadhi nchini Ethiopia katika kambi nne ( Kule, Lietchuor, Pugnido na Okugo) na wengine 9.600 wamepewa hifadhi katika maeneo yaliyo karibu na mipaka ya nchi hio na mataifa jirani.

Waasi wa Sudani Kusini wakiwa katika mazoezi ya kijeshi
Waasi wa Sudani Kusini wakiwa katika mazoezi ya kijeshi © RFI/Stéphanie Braquehais

Wakati mapigano yakiendelea nchini Sudan Kusini, huku msimu wa mvua ukikaribia, mashirika yanayohudumia wakimbizi yamekua yakiandaa mazingira mazuri ya kuwapokea wakimbizi na tayari yameanza kutuma mahema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.