Pata taarifa kuu
Jamhuri ya Afrika ya Kati- Haki za binadamu

CAR: viongozi wa kidini wayashushia lawama makundi ya Seleka na Anti-balaka

Maaskofu wa makanisa mbalimbali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wameyatuhumu makundi ya Seleka na Anti-Balaka kuwa chanzo cha kuendelea kuzorota kwa hali ya usalama kwenye taifa hilo ambalo linakabiliwa na changamoto ya mauji ya kidini.

Waislamu waliyoyahama makaazi yao wakihofiwa kuuawa na wanamgambo wa kundi la Anti-balaka wakisubiri kwenye uwanja wa ndege wa Bangui kusafirishwa hadi Chad.
Waislamu waliyoyahama makaazi yao wakihofiwa kuuawa na wanamgambo wa kundi la Anti-balaka wakisubiri kwenye uwanja wa ndege wa Bangui kusafirishwa hadi Chad. AFP PHOTO/ ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Maaskofu hawa wanadai kuwa makundi kama vile ya Seleka, Anti-Balaka, Fulani na kundi la LRA la nchini Uganda yamekuwa yakijichukulia sheria mkononi kwa kutekeleza mauaji dhidi ya raia wanaowakamata.

Mpiganaji wa kundi la anti-balaka, mjini Bangui, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Februari 22 mwaka 2014.
Mpiganaji wa kundi la anti-balaka, mjini Bangui, nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, Februari 22 mwaka 2014. REUTERS/Luc Gnago

Licha ya sehemu kubwa ya mauaji ya kiholela kudhibitiwa mjini Bangui, bado maeneo mbalimbali ya nchi yemeendelea kushuhudia uwepo wa matukio ya unyanyasaji, mateso na mauji dhidi ya raia yanayofanywa na makundi haya, ambapo viongozi wa dini sasa wanataka makundi hayo kukomesha vitendo vya kikatili.

Mpiganaji wa zamani wa kundi la zamani la waasi wa Seleka akiwa kando ya barabara inayoelekea mji wa Bambari, ambako raia wanasema kushambuliwa mara kwa mara na anti-Balaka.
Mpiganaji wa zamani wa kundi la zamani la waasi wa Seleka akiwa kando ya barabara inayoelekea mji wa Bambari, ambako raia wanasema kushambuliwa mara kwa mara na anti-Balaka. REUTERS/Siegfried Modola

Wachambuzi wa mambo wanasema kauli hii ya maaskofu ni ya kupongezwa, kwani makundi haya ya Seleka na Anti-balaka hayana nguvu, bali chuki kati ya raia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati imepandikizwa kidini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.