Pata taarifa kuu
DRC-PRETORIA-Sheria

Afrika Kusini : Pretoria : Kesi kuhusu jaribio la mapinduzi DRC yaanza kusikiliza

Kesi ya watuhumiwa 20 raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wa jaribio la kuipindua serikali ya rais Joseph Kabila itaanza kusikilizwa hii leo mjini Pretoria.

Kesi ya watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi ya serikali ya joseph Kabila.
Kesi ya watuhumiwa wa jaribio la mapinduzi ya serikali ya joseph Kabila. AFP PHOTO / STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Watuhumiwa hao wa vuguvugu la “Union des nationalistes pour le renouveau” UNR walikamatwa mwaka uliopita baada ya kufwatiliwa kwa muda mrefu na polisi ya Afrika Kusini katika harakati zao za kupanga njama za mapinduzi dhidi ya serikali ya Kinshasa.

Mahakama nchini Afrika Kusini inadai kushikilia ushahidi wa kutosha wa njama hiyo kwa kumpenyeza askari polisi mmoja katika kundi hilo kwa miezi na kwa kunasa barua pepe kadhaa za mawasiliano yao pamoja na orodha ya vifaa na silaha walivyoagiza.

Kwa mujibu wa hati ya mashtaka, orodha ya watu waliopangwa kuuawa katika mapinduzi hayo ilipatikana katika kompyuta mmoja ya watuhumiwa, jina la rais Joseph Kabila likitajwa kama mmoja wa viongozi ambao wanalengwa.

Etienne Kabila adai kwamab aaliondoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2002 akihofia usalama wake.
Etienne Kabila adai kwamab aaliondoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwaka 2002 akihofia usalama wake. AFP PHOTO / STRINGER

Raia wa DRC Etienne Kabila ni mmoja wa viongozi wa operesheni hiyo ambayo kwa mujibu wa waangalizi wengi huenda wakapewa adhabu ya kufungo cha maisha jela pamoja na kurejeshwa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo baada ya kesi inayotarajiwa kudumu muda wa majuma sita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.