Pata taarifa kuu
DRC-Ebola-Afya

Serikali ya Congo yathibitisha watu 6 kuambukizwa virusi vya Ebola

Umoja wa Mataifa umetangaza siku ya jumatano kutenga msaada wa dola za kimarekani milioni moja na laki tano kuisaidia Jamhuri ya Kidemo krasia ya Congo kupambana na virusi vya Ebola, siku chache tu baada ya nchi hiyo kuthibitisha kuwepo kwa virusi hivyo nchini Congo.

Watu sita waambukizwa virusi vya Ebola katika mkoa wa Equateur, nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Watu sita waambukizwa virusi vya Ebola katika mkoa wa Equateur, nchini jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Luis Encinas/MSF
Matangazo ya kibiashara

Wakati hayo yakijiri, serikali ya Congo imethibitisha jumla ya maambukizi sita baada ya vipimo vilivyofanywa kwenye maabara ya mjini Franceville nchini Gabon na kuwaomba watu wawe watulivu kwa vile aina ya Ebola nchini humo ni tofauti na ile ya Afrika magharibi.

“Pesa hizo zimetolewa ili kukabiliana na hali ya dharura”,kaimu msemaji wa tume ya Umoja wa Mataifa nchini Congo, Monusco, Carlos Araujo katika mkutano na waandishi wa habari.

Katika hali ya kupambana na virusi vya Ebola ambavyo vimesababisha vifo vya watu 13 tangu Agosti 11 katika mkoa wa Equateur, serikali ya Congo imeiomba msaada jumuiya ya kimataifa.

Serikali ya Congo inahitaji pesa zinazo kadiriwa kuwa sawa na Dola milioni 4.5, huku Dola milioni 2 zikihitajika haraka iwezekanavyo.

Hata hivo, imekua vigumu kufikisha dawa za kupambana na Homa ya Ebola katika eneo kunakoripotiwa ugonjwa huo kutokana na ubovu wa miondombinu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.