Pata taarifa kuu
RWANDA-RCN-FDLR-Sheria-Siasa

Rwanda: kesi inayowakabili maafisa wastaafu yaahirishwa

Mahakama ya kijeshi imeahirisha Ijumaa wiki hii kusikilizwa kwa kesi inayowakabili Brigedia Jenerali Frank Rusagara, Kanali Tom Byabagamba na Kapteni Kabuye hii leo. Kesi hiyo itasikilizwa Septemba 5 mwaka 2014.

Jenerali Frank Rusagara (kulia) na kolonel Tom Byabagamba (kushoto) mbele ya Mahakama ya kijeshi ya Rwanda.
Jenerali Frank Rusagara (kulia) na kolonel Tom Byabagamba (kushoto) mbele ya Mahakama ya kijeshi ya Rwanda. RFI/Bryson Bichwa
Matangazo ya kibiashara

Watatu hao walitiwa nguvuni wiki jana kwa tuhuma za kuhatarisha usalama wa taifa.
Rusagara na Kabuye walistaafu mwaka jana, baada ya kulitumikia jeshi la Rwanda (RDF).

Tom Byabagamba alikamatwa siku chache tu tangu arudi kutoka Sudani alikokuwa amekwenda katika operesheni ya kurejesha amani katika taifa hilo lenye mzozo,na aliwahi kuwa mkuu wa kikosi cha ulinzi wa rais Paul Kagame.

Jenerali Frank Rusagara akiwa na mawakili wake.
Jenerali Frank Rusagara akiwa na mawakili wake. RFI/Bryson Bichwa

Brigedia Jenerali Frank Rusagara alichukua nyadhifa tofauti jeshini kwa nyakati tofauti kabla ya kuteuliwa kuwa mwambata katika ubalozi wa Rwanda nchini Uingereza akihusika na maswala ya jeshi.

Msemaji wa jeshi la Rwanda, Joseph Nzabamwita, amesema Rusagara, Kabuye na Byabagamba wameshtakiwa pamoja.

Hayo yakijiri Mahakama ya kijeshi nchini imeahirisha pia uamuzi wake katika kesi ya "ugaidi" na "kupanga njama" dhidi ya rais Paul Kagame inayomkabili Luteni Joel Mutabazi, afisa wa zamani wa kikosi cha ulinzi wa rais wa Rwanda alikamatwa na kutumwa Rwanda na serikali ya Uganda Oktoba 2013 licha ya hali yake ya ukimbizi.

"Upande wa utetezi umeomba Mahakama kutafuta baadhi ya ushahidi, ambao tunaouchukulia ni muhimu kwa kuufanyia kazi kabla ya uamuzi kutolewa”, amesema Jaji kiongozi, Kamanda Bernard Rugamba Hategekimana.

Joël Mutabazi (kushoto) akiwa mahakamani pamoja na watuhumiwa wezake.
Joël Mutabazi (kushoto) akiwa mahakamani pamoja na watuhumiwa wezake. AFP PHOTO/ Stéphanie Aglietti

Joel Mutabazi na watuhumiwa wenzake 15, kwa mujibu wa upande wa mashtaka, walishiriki kwa viwango tofauti katika mashambulizi ya gruneti yaliyotekelezwa nchini Rwanda tangu mwaka 2010. Serikali ya Kigali ilikituhumu chama cha upinzanicha RCN kiliyo uhamishoni pamoja na waasi wa kihutu wa Rwanda (FDLR) kuhusika na mashambulizi hayo.

"Sheria inaruhusu mahakama kufanya uchunguzi wa kina na kuonesha ushahidi mpya," amesema Kamanda Hategekimana, huku akiahirisha kesi hiyo kusikilizwa kwa mara nyingine Septemba 12.

Mwishoni mwa mwezi Julai, upande wa mashtaka uliomba kifungo cha maisha jela dhidi ya Mutabazi, ambaye anatuhumiwa tangu mwezi Januari "kuunda kundi la watu wenye silaha, kupanga njama dhidi ya rais, ugaidi, kupanga njama dhidi ya serikali iliyochaguliwa na wananchi, kueneza taarifa za uongo kwa lengo la kujenga chuki kati mataifa mbalimbali na serikali Rwanda, kumiliki silaha za moto kinyume cha sheria pamoja na utoro jeshini.

Joel Mutabazi na mtuhumiwa mwenza mmoja waliombewa na mahakama kifungo cha maisha jela, miaka 37 gerezani dhidi ya wengine tisa, miaka 20 jela dhidi ya wawili, miaka saba dhidi ya ndugu mdogo wa Joel Mutabazi na hukumu ya miaka mitano dhidi ya mjomba wake na mke wa kaka yake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.