Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-PISTORIUS-Sheria

Afrika Kusini: Oscar Pistorius aendelea kunufaika na dhamana

Kwa mujibu wa jaji wa mahakama ya mji wa Pretoria nchini Afrika Kusini, Thokozile Masipa, Oscar Pistorius hana hatia ya kumuua Reeva Steenkamp, mauaji ambayo yalitokea Februari 14 mwaka 2013. Hata hivo haimaanishi kuwa mwanariadha huyo hatohukumiwa.

Mahakama yafuta tuhuma ya mauaji iliyokua inamkabili mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, Septemba 11 mwaka 2014.
Mahakama yafuta tuhuma ya mauaji iliyokua inamkabili mwanariadha wa Afrika Kusini, Oscar Pistorius, Septemba 11 mwaka 2014. REUTERS/Siphiwe Sibeko
Matangazo ya kibiashara

Tangazo hilo limetolewa alhamisi wiki hii mchana : Jaji amebaini kwamba Oscar

Oscar Pistorius alimfyatulia risase mpenzi wake Reeva Steenkamp kupitia mlango huu.
Oscar Pistorius alimfyatulia risase mpenzi wake Reeva Steenkamp kupitia mlango huu. REUTERS/Alexander Joe/Pool

hana hatia ya mauaji. Kwa kutetea uamzi wake, hakimu huyo ameeleza kwamba kuna tofauti kati ya kufyatua risase na kuwa na nia ya kuua. Je mwanariadha huyo alikua na nia ya kuua mpenzi wake wakati alipofyatua risase kwenye mlango wa choo? Mwanariadha alikanusha mwenyewe na kusema kwamba alifyatua risase kwenye mlango wa choo baada ya kusikia mtu chooni akidhani kwamba ni mtu ambaye alikua amekuja kuhatarisha usalama wake.

Mku wa kikosi cha usalama nchini Arfika kusini, Pieter Baba, akitoa ushahidi wake katika kesi ya Oscar Pistorius, mjini Pretoria, Machi 07 mwaka2014.
Mku wa kikosi cha usalama nchini Arfika kusini, Pieter Baba, akitoa ushahidi wake katika kesi ya Oscar Pistorius, mjini Pretoria, Machi 07 mwaka2014. REUTERS/Schalk van Zuydam/Pool

Maswali yote yako wazi, je alikua na dhamira ya kuua? Jaji, Thokozile Masipa, amebaini hapana, kwa sababu ya mwenendo wake aliyouonesha muda mfupi baada ya tukio hilo : alipigia sim vyombo vya usalama, wakati huo huo alimpigia sim daktari ili aweze kuwasili eneo la tukio na kumfanyia matibabu mpenzi wake huyo wa zamani ambaye alimfyatuliwa risase bila kukusudia. Muda mchache uliyofuata, alibaini kwamba alikua alijidanganya, hakua na nia ya kumuua. Jaji amesema kutokana na hali ya uzuni aliyokua nayo, Oscar hangelikumbuka katika utetezi wake kusema yote aliyoyafanya akijaribu kuokoa maisha ya Reeva Steenkamp.

Kutokana na utetezi wake, Oscar Pistorius hakupatikana na hatia yakuua kwa kukusudia. Saa moja kabla, jaji alitupilia mbali hoja ya kuua bila kukusudia iliyotolewa na mwendeshamashtaka dhidi ya Oscar. Kinachosalia kwa sasa ni hukumu dhidi ya kuua bila kukusudia au kuachiliwa huru. Lakini hata hivo, sheria ya jinai ya Afrika Kusini haiweki wazi hukumu ya kosa la kuua bila kukusudia. Hukumu imetolewa, lakini huenda Pistorius akapewa adhabu ya kufungwa jela au adhabu ya kifungo jela ikiwa ni pamoja na faini. Jaji Thokozile Masipa amesema adhabu hiyo itatolea Oktoba 13 mwaka 2014.

Jaji Masipa ametupilia mbali ombi la mashtaka la kutaka dhamana ya Pistorius ibatilishwe, na kubaini kwamba upande wa mashtaka haukuonesha umuhimu wowote wa kubatilisha dhamana hiyo na badala yake ameongeza muda hadi pale uamzi wa adhabu urtakapochukuliwa.

Wakati hakimu alipotangaza kufuta tuhuma ya mauaji, Pistorius ameangua kiliyo, huku akitokwa na machozi mengi kizimbani.

Oscar Pistorius mwanariadha aneishi na ulemavu.
Oscar Pistorius mwanariadha aneishi na ulemavu. REUTERS/David Gray

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.