Sierra Leone: maambukizi ya Ebola yadhibitiwa
Serikali nchini Sierra Leone, inasema imefanikiwa pakubwa kudhibiti maambukizi mapya ya ugonjwa hatari wa Ebola baada ya amri ya siku tatu ya raia wa nchi hiyo kutotoka nje kumalizika saa sita usiku jana Jumapili.
Imechapishwa:
Sierra Leone ni mojawapo ya mataifa ya Afrika Magharibi ambayo yanakabiliwa na Ebola, na raia wake 550 wamepoteza maisha huku wengine wakifariki kutoka Liberia na Guinea.
Kwa kipindi hicho cha siku tatu, maafisa wa afya walizuru makaazi ya raia nchini humo na kutoa elimu ya namna ya kujizuia na maambukizi ya Ebola.
Shirika la afya duniani WHO linasema haya ndio maambukizi makubwa kuwahi kushuhudiwa duniani.
Mlipuku huo wa Homa ya Ebola umesababisha vifo vya watu 2600 katika nchi za Sierra Leone na Liberia tangu mwanzoni mwa mwaka 2014, na kusababisha mataifa hayo mataifa hayo kukabiliwa na mdororo wa kiafya ambao umeathiri sekta za jamii na uchumi.
Nchini Sierra Leone ambako Homa ya Ebola imewaua watu 562, raia milioni sita wa taifa hilo walitakiwa kubaki nyumbani kwa siku tatu mfululizo tangu ijumaa hadi jana jumapili. Operesheni hiyo imeendeshwa na watu 30,000 ambao walijitolea.
Watu 22 wamekutwa wameambukizwa virusi vya Ebola kufuatia operesheni hiyo ya siku tatu katika jimbo la magharibi, mji wa Freetown ikiwa ni moja ya sehemu ya jimbo hilo.
Naibu kiongozi wa idara ya afya, Saria Kamara, amesema watu kati ya 60 na 70 wamefanyiwa mazishi hivi karibuni kutokana na Homa aya Ebola.