Pata taarifa kuu
Cameroon-Nigeria

Boko haram yaachia mateka 27 akiwemo mke wa naibu waziri mkuu Cameroon

Watu 27 wakiwemo raia 10 wa China waliokuwa wakishikiliwa na kundi la kiislamu la Boko Haram wamewasili huru katika mji mkuu wa Cameroon.

Mke wa naibu waziri mkuu Amadou Ali alikuwa miongoni mwa mateka wa wapiganaji wa Boko Haram
Mke wa naibu waziri mkuu Amadou Ali alikuwa miongoni mwa mateka wa wapiganaji wa Boko Haram globalpost.com
Matangazo ya kibiashara

Mateka hao walisafirishwa hadi Yaounde wakitokea eneo la mbali kaskazini baada ya kuachiwa huru mapema jana.

Miongoni mwa mateka hao ni mke wa naibu waziri mkuu Amadou Ali.

Watu hao walitekwa katika mashambulizi mawili tofauti la mwezi may na Julai jirani na mpaka wa Cameroon na Nigeria,na haijafahamika kwa namna gani wameachiliwa huru.

Wapiganaji wa Boko Haram wanapigania kuwepo na serikali ya kiislamu nchini Nigeria licha ya wapiganaji wake mara kwa mara kuvuka mpaka na kuingia Cameroon.

Raia wengi wa Nigeria waishio miji ya mipakani wamehamia Cameroon kukimbia mashambulizi ya wapiganaji hao ambayo yamekuwa ya mara kwa mara katika miezi ya hivi karibuni.

Mnamo mwezi Julai mataifa ya Cameroon, Nigeria, Chad na Niger yalikubaliana kuunda jeshi la kanda hio litakalokabiliana na kundi hilo la kiislamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.