Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA

Majeshi ya Ufaransa yafurusha wapiganaji wa jihadi Mali,yaua 24

Majeshi ya Ufaransa yamewashambulia wapiganaji 24 wa kiislamu na kuwaua huku silaha kadhaa zikidhibitiwa kutoka kwa wapiganaji hao kufuatia oparesheni kubwa kaskazini mwa Mali ambako majeshi ya Ufaransa yalingia mwaka jana kukomesha uasi wa kiislamu.

Harakati za ukombozi wa Mali zinasimamiwa na jeshi la kimataifa la MINUSMA kumaliza makundi ya kigaidi nchini humo
Harakati za ukombozi wa Mali zinasimamiwa na jeshi la kimataifa la MINUSMA kumaliza makundi ya kigaidi nchini humo MINUSMA/Marco Dormino
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya jeshi la ufaransa imefafanua kuwa oparesheni iliyoanza 28 mwezi Octoba na kumalizika ijumaa ilifanikisha kuwaua wapiganaji wa kiislamu 24 na kuwatia nguvuni wengine 2.

Magari kadhaa yaliharibiwa wakati silaha na vifaa vya kutengenezea vilipuzi vikidhibitiwa na wanajeshi wa Ufaransa.

Oparesheni iliyofanyika katika eneo la Kidal imedhoofisha mtandao wa magaidi kaskazini mwa Mali.

Askari mmoja wa jeshi la ufaransa aliuawa 28 octoba ikiwa ni katika sehemu ya makabiliano yaliyolenga kumaliza kurejea tena kwa waiganaji wa kijihadi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.