Pata taarifa kuu
SENEGAL-AFRIKA-MKUTANO-USALAMA-AMANI

Usalama Afrika wawakusanya viongozi wengi Dakar

Mkutano wa kwanza kuhusu amani na usalama barani Afrika umezinduliwa Jumatatu Desemba 15 katika mji mkuu wa Senegal, Dakar.

Kituo cha kimataifa cha mikutano ambako kunafanyika mkutano kuhusu amani na usalama, mjini Dakar nchini Senegal..
Kituo cha kimataifa cha mikutano ambako kunafanyika mkutano kuhusu amani na usalama, mjini Dakar nchini Senegal.. RFI/Paulina Zidi
Matangazo ya kibiashara

Lengo la mkutano huu ni kuwahimiza viongozi wa Afrika kuhusu ongezeko la wanajihadi katika maeneo ya kusini mwa jangwa la Sahara pamoja na wapiganaji wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Jean-Yves Le Drian ameshiriki mkutano huu pamoja na marais wengi kutoka bara la Afrika.

Kamishna wa taasisi ya Umoja wa Afrika kwa ajili ya amani na usalama, Smain Chergui, ndiye ambaye alifungua mkjutano huu. Alikumbusha wajibu kwa Afrika na raia wa Afrika kwa kuwa makini kuhusu suala la usalama barani Afrika.

“ Afrika inaweza kua kitovu cha uchumi duniani iwapo tutawajibika kuzidisha juhudi katika sekta ya usalama na kuheshimu haki za binadamu”, amesema Smain Chergui,

Baadaye Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, alipata fursa ya kuelezea wale wote ambao wamekua wakitiwa mashaka kuhusu ufaransa kuwa na majukumu ya kulinda usalama Afrika. Jean-Yves Le Drian amekaribisha mchango mkubwa unaotolewa na kikosi cha Umoja wa Afrika kwa kurejesha amani na usalama katika baadhi ya mataifa barani Afrika.

“ Sudani, Somalia na kwingineko, ni sauti ya Umoja wa Afrika ambayo imekua ikisikika”, ameendelea kusema Waziri wa ulinzi wa Ufaransa.

Jean-Yves Le Drian amebaini kwamba Ufaransa inachangia katika jitihada hizo kwa kuimarisha usalama barani Afrika. Suala la usalama linawahusu kwa njia moja ama nyingine raia wa Afrika wenyewe.

Waziri wa ulinzi swa Ufaransa amezungumzia pia kuhusu hali inayojiri nchini Libya. Amesema kutiwa wasiwasi na tishio la mdororo wa usalaama unotokea kusini mwa Libya.

Jean-Yves Le Drian, amezungumzia pia tishio la kundi la Boko Haram, akibaini kwamba kwa sasa Boko haram si tishio tu kwa Nigeria au kanda nzima, ni tishio kwa ulimwengu mzima.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.