Pata taarifa kuu
TANZANIA-KENYA-BISHARA-MAZINGIRA

Muuzaji wa pembe za ndovu akamatwa Tanzania

Mtu anaye tuhumiwa kuwa kiongozi wa mtandao wa biashara ya pembe za ndovu amekamatwa nchini tanzania.

Saisie de défenses d'éléphants au Kenya. Le braconnage est en constante augmentation dans ce pays.
Saisie de défenses d'éléphants au Kenya. Le braconnage est en constante augmentation dans ce pays. Harambee Kenya
Matangazo ya kibiashara

Feisal Mohamed Ali, raia wa Kenya amekamatwa na polisi ya kimataifa ya Interpol katika mji mkuu wa Tanzania, Dar es Salaam.

Kwa muda wa miezi sita wachunguzi wamekua wakifuatilia shughuli ya mfanyabiashara huyo. Polisi ya kimataifa ya Interpol ilimuweka Feisal Mohamed Ali kwenye orodha ya watu tisa wanaotafutwa duniani kwa uhalifu dhidi ya mazingira.

Feisal Mohamed Ali, mwenye umri wa maika 47, anasadikiwa kumiliki ghala la injini za magari lililogunduliwa Juni 5 mwaka 2014 katika mji wa pili wa Kenya. Zaidi ya tani mbili za pembe za ndovu ziligunduliwa ndani ya ghala hilo. Watu waliokua wakishirikiana na mfanyabiashara huyo walikamatwa, lakini Feisal Mohamed Ali alifaulu kutimka.

Feisal Mohamed Ali, amekatwa katika mji wa Dar es Salaam, baada ya miezi sita akitafutwa na polisi ya Kenya. Tanzania na Kenya ni nchi ambazo zimekua zikilengwa na biashara haramu ya pembe za ndovu ambapo pembe hizo za ndovu zimekua zikisafirishwa hadi barani Asia.

Tangu mwezi Oktoba polisi ya kimataifa ya Interpol ilianzisha operesheni katika nchi 36 duniani ya kuwasaka watu wanahusika na uhalifu wa mazingira. Operesheni hiyo inalenga watu 139 wanaoshukiwa kuendesha uvuvi kinyume cha sheria, biashara ya baadhi ya viungo vya wanyama pori, aidha uhalifu mwengine unaoambatana na uharibifu wa mazingira.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.