Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBi-SAISA

Maneno ya Moise Katumbi yaibua hisia tofauti kwa wanasiasa

Maneno machache aliyotamka mkuu wa mkoa wa Katanga Moise Katumbi Chapwe yamezua hisia tofauti katika jamii ya wanasiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Maneno ya Moise Katumbi yamefananishwa kama onyo kwa rais Joseph Kabila.
Maneno ya Moise Katumbi yamefananishwa kama onyo kwa rais Joseph Kabila. www.katanga.cd
Matangazo ya kibiashara

Aliporejea mjini Lubumbashi hivi karibuni, baada ya miezi miwili akiwa nje ya nchi kwa matibabu, Moise Katumbi alitoa mfano wa mechi inayozikutanisha timu mbili za soka, ambapo alisema watazamaji wanaweza kukubali hatua inayochukuliwa na mwamzi wa kuiadhibu timu fulani kwa mikwaju miwili ya penalti, lakini mkwaju wa tatu unaweza kusababisha watazamaji kuingia uwanjani na kupinga uamzi huo.

Wengi wamefananisha maneno hayo kama onyo alilolitoa dhidi ya rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Joseph Kabila, ambaye anakaribia kumaliza muhula wake wa pili uanokubaliwa na katiba ya Congo.

Chama cha UNC kimepongeza kwamba idadi ya wanaopinga muhula wa tatu kwa Joseph Kabila imeendelea kuongezeka.

“ Ni hatua kubwa kuona mkuu wa mka anakozaliwa rais Kabila, anapinga kugombea kwa rais huyo muhula wa tatu”, amesema Vital Kamerhe, kiongozi wa chama cha upinzani cha UNC.

“Siku za kabila kuondoka madarakani zimeanza kuhesabiwa, tulidhani kwamba ndugu zake kutoka mkoa wa Katanga watamuunga mkono, kumbe sivyo”, amesema kwa upande wake, katibu wa kitaifa anaye husika na masuala ya nje katika chama cha UDPS.

Kwa mujibu wa Martin Fayulu kutoka chama cha FAC, kulingana na maneno hayo ya Moise Katumbi, ni wazi kwamba hashirikiani tena na vyama vinavyounga mkono utawala wa chama cha PPRD. Martin Fayulu amebaini kwamba vigogo katika chama tawala cha PPRD cha rais Kabila wameanza kujiondoa mmoja baada ya mwengine.

Kiongozi wa chama cha mshikamano kwa kwa raia wa Congo kwa ajili ya Demokrasia (SCD), Jean-Claude Muyambo, amebaini kwamba maneno ya Moise Katumbi ni kama wito kwa raia wa kupinga rais kabila kugombea urais kwa muhula wa tatu.

Upande wa chama tawala na washirika wake wamesema watatoa msimamo wao siku za hivi karibuni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.