Pata taarifa kuu
CAMEROON-NIGERIA-BOKO HARAM--Usalama

Boko Haram yatimuliwa Achigachia

Hali ya utulivu imerejea katika mji wa Achigachia kaskazini mwa Cameroon kwenye mpaka na Nigeria, baada ya siku nzima ya mapigano Jumapili Desemba 28 mwaka 2014 kati ya wanamgambo wa kundi la Boko Haram na jeshi la Cameroon.

wanamgambo wa kundi la boko Haram wamekua wakizidisha mashambulizi katika eneo la mpaka wa Cameroon na Nigeria.
wanamgambo wa kundi la boko Haram wamekua wakizidisha mashambulizi katika eneo la mpaka wa Cameroon na Nigeria. AFP PHOTO/REINNIER KAZE
Matangazo ya kibiashara

Wapiganaji wameweza kupenya na kuingia katika kambi ya kijeshi kwa masaa kadhaa kabla ya kujiondoa baada ya ndege ya jeshi ya Cameroon kuanzisha mashambulizi ya anga. Haijaelezwa hasara iliyotokana na mapiganao hayo, lakini wanamgambo wa kundi la Boko Haram wamesababisha hofu katika maeneo wakipokua wakipita, na kupelekea maelfu ya raia kuyahama makaazi yao.

 

Msemaji wa jeshi la Cameroon, kanali Badjek, amesema kuwa ni kwa mara ya kwanza jeshi la Cameroon linatumia ndege dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram. Uamuzi huo wa kutumia ndege umechukuliwa na rais, Paul Biya mwenyewe.

Awali msemaji wa jeshi la Cameroon amebaini kwamba watatumia ndege ili kuwatimua wanamgambo wa Boko Haram.

" Tulijua kwamba [adui] alitaka kututeka katika njia zote. Kwa hiyo, nadhani kwamba utumiaji wa ndege ni muhimu sana kwa sisi kushinda si tu kuwatimua wanamgambo wa Boko lakini pia kuwa na utaratibu mwengine katika uwanja wa mapigano", amesema kanali Badjek .

" Tulipendelea kutumia ndege ili kupunguza idadi ya vitu ambavyo vinaweza kuharibiwa kutokana na mapigano. Lakini kutokana na kuwa adui amekua ameshakaguliwa kijiografia, nadhani tutatumia jeshi la anga. Huu ni utaratibu mpya ambao tumeanza kutumia ili kulidhibiti kundi la Boko Haramu", ameongeza kanali Badjek.

Wapiganaji wa Boko Haram kabla ya kuondoka katika kambi hiyo ya jeshi walipora vifaa vyote viliyokuwemo katika kambi hiyo mkiwemo na silaha. Idadi ya vifo kutokana na mapigano hayo haijatolewa, lakini kulingana na vyanzo vya kijeshi kwenye emeo hilo, huenda watu wengi waliuawa katika mapigano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.