Pata taarifa kuu
GAMBIA-MAPINDUZI-SIASA

Jaribio la mapinduzi Gambia

Mkanganyiko umejitokeza nchini gambia kuhusu hali katika mji mkuu wa nchi hio Banjul, ambapo milio ya risasi ilisikika mapema Jumanne asubuhi.

Yahya Jammeh katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Septemba 25 mwaka 2014.
Yahya Jammeh katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa, Septemba 25 mwaka 2014. Reuters/Lucas Jackson
Matangazo ya kibiashara

Vyanzo mbalimbali vimesema kuwa Ikulu ya rais imeshambuliwa wakati ambapo rais Yahya Jammeh yuko ziiarani ugenini. Jaribio hilo la mapinduzi limeendeshwa na baadhi ya wanajeshi wa serikali.

Afisa katika jeshi ambaye amenukuliwa na shirika la habarai la Ufaransa AFP, amethibitisha kwamba polisi na jeshi vemedhibiti hali ya mambo.

Vyanzo vya kimagharibi vimebaini kwamba jaribio la mapinduzi limezimwa, na kusema kuwa kikosi cha wanajeshi wanaomuunga mkono rais kimedhibiti hali ya mambo.

Kwa sasa, viongozi au kundi la wanajeshi lililitaka kuipindua serikali. hawajajieleza kuhusu tukio hilo. Rais Yaya Jammeh, yuko ziarani nje ya nchi.

Haijulikani ni akina nani ambao walihusika katika tukio hilo. Vyanzo vya kidiplomasia vimebaini kwamba wanajeshi wa kikosi cha ulinzi wa taifa wameshiriki katika jaribio hilo la mapinduzi.

Redio ya taifa ilisitisha matangazo yake kwa muda wa masaa kadhaa, huku kukionekana askari wengi mitaani wakipiga doria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.