Pata taarifa kuu
MALI-UN-USALAMA

Maandamano ya watu wenye hasira Kidal

Hali ya wasiwasi inaripotiwa kaskazini mwa Mali. Wanajeshi wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo (Minusma), walifyatua risasi Jumanne wiki hii kwenye ngome za makundi yenye silaha katika mji wa Tabankort.

Askari wa Minusma wakitoa walinzi mbele ya ofisi ya jimbo la Kidal, Novemba 15 mwaka 2013.
Askari wa Minusma wakitoa walinzi mbele ya ofisi ya jimbo la Kidal, Novemba 15 mwaka 2013. Des soldats de la Minusma montent la garde devant le gouvernorat
Matangazo ya kibiashara

Kikosi hicho cha Umoja wa Mataifa kilibaini kwamba kilijibu mashambulizi ya makundi hayo yenye silaha dhidi yao.

Hayo yakijiri maandamano ya watu wenye hasira yamefanyika Jumatano Januari 21 katika mji wa Kidal, huku pande mbili zikitofautiana kuhusu kilichotokea.

Kwa upande wake kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali kimesema watu wenye silaha waliokua ndani ya gari ndogo walifyatulia risasi kwenye ngome zao, na wao hawakusita kujibu mashambulizi hayo. Lakini kiongozi mmoja wa MNLA amethibitisha kwamba helikopta ya kikosi cha Umoja wa Mataifa ndio iliyofyatua risasi kwenye ngome zao.

Kidali, mji ambao uko kwenye umbali wa kilomita zaidi ya 100 na Tabankourt, ulishuhudiia miili ya watu waliouawa na wengine kujeruhiwa wakiletwa Jumanne jioni wiki hii, jambo ambalo limewatia ghadhabu raia wa mji huo, ambao wamedai kuwa wapiganaji 11 ndio waliuawa na wengine 21 wamejeruhiwa.

Jumatanu Januari 21 asubuhi, mamia kwa maelfu ya watu walikusanyika katika uwanja wa ndege, ambapo walikua wakiimba na kusema : “ Azawad ndio, Minusma hapana”.

Nyaya za kulinda eneo wanakopiga kambi wanajeshi wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Mali ziliondolewa na raia, huku wakichoma moto jenereta. Askari wa Umoja wa Mataifa walilazimika kutumia mabomu ya kutoa machozi, kabla ya raia hao kuondoka.

Baadae mchana mkutano ulifanyika nyumbani kwa kiongozi wa kimila. Afisa wa Ufaransa wa kikosi cha Barkhane alikuwepo katika mkutano huo. Kiongozi huyo baadae alijielekeza kwenye uwanja wa ndege ili kuwasihi waandamanji kurejea nyumbani na kuwa watulivu.

Hata kama hali ya utulivu imerejea, uhusiano kati ya Minusma na makundi yenye silaha umeonekana kuvunjika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.