Pata taarifa kuu
DRC-JAMII-USALAMA-HAKI

Kaburi la pamoja la Maluku laibua mjadala

Kugunduliwa kwa kaburi la pamoja la Maluku, ambako ilizikwa miili ya watu 421 usiku wa tarehe 19 Machi, kumeibua maswali mengi kuhusu mauaji ya watu kadhaa wakati wa maandamano ya mwezi Januari mwaka 2015 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Makaburi ya Maluku, ambapo miili ya watu 421 ilikozikwa katika kaburi la pamoja, usiku wa Machi 19 mwaka 2015.
Makaburi ya Maluku, ambapo miili ya watu 421 ilikozikwa katika kaburi la pamoja, usiku wa Machi 19 mwaka 2015. AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA
Matangazo ya kibiashara

Viongozi wa mkoa wamebaini kwamba miilli hio ni ya watu wasiojiweza ambao walifariki na baadaye kuwekwa katika vyumba vya kuhifadhi maiti mjini Kinshasa kwa muda mrefu.

Kutokana na utata ambao umeibuka baada ya kugunduliwa kwa kaburi hilo la pamoja, viongozi wa mkoa walikutana Jumanne wiki hii na vyombo vya habari, ili kuthibitisha kwa mara nyingine tena kauli yao ya mwanzo, kwamba ni miili ya watu wasiojiweza ambayo ilikua katika vyumba vya kuhifadhi maiti kwa muda mrefu mjini Kinshasa.

Tukio hili la kuzika miili ya watu katika kaburi la pamoja si la kwanza. Ni zoezi ambalo lilikuepo na bado linaendelea, katika hali ya kupunguza miili ya watu katika chumba cha kuhifadhi maiti cha mji wa Kinshasa, ambacho kina uwezo wa kupokea miili ya watu 300, viongozi wa mkoa wamethibitisha. Hili zoezi ni la nne katika kipindi cha mwaka mmoja.

Kaburi hili la pamoja la Maluku ililikozikwa miili ya watu 421, ni mbali kidogo na mji wa Kinshasa karibu kilomita 100 na mji huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.