Pata taarifa kuu
BURUNDI-SIASA

Mashirika ya kiraia yaapa kuingia mitaani Burundi

Wakati chama tawala nchini Burundi cha Cndd-Fdd kikitazamiwa kumtangaza mgombea wake katika uchaguzi ujao wa urais Jumamosi wiki hii, vyama vya kiraia vimewatolea wito raia kuandamana Jumapili asubuhi iwapo chama hicho kitamtangaza rais Pierre Nkurunziza kama mgombea wake.

Pacifique Nininahazwe, mmoja kati ya wanaharakati wa mashirika ya kiraia Burundi.
Pacifique Nininahazwe, mmoja kati ya wanaharakati wa mashirika ya kiraia Burundi. /kiyago.unblog.fr
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanajiri wakati viongozi mbalimbali wa chama tawala cha Cndd-Fdd katika ngazi ya taifa wamekua wakiwatolea wito wafuasi wa chama hicho kwamba mgombea katika uchaguzi wa urais kwa tiketi ya chama cha Cndd-Fdd ni rais Pierre Nkurunziza.

Jumatatu jioni wiki hii, serikali kupitia mawaziri wake wanne, ulinzi usalama, mambo ya ndani na sheria, ilitoa onyo kali kwa wale watakaoandamana kinyume cha sheria kwamba watachukuliwa hatua za kisheria.

Tishio hilo la mashirika ya kiraia linakuja wakati upinzani umeendelea kupinga nia ya rais Nkurunziza ya kombea muhula wa tatu.

Tangu majuma mawili yaliyopita viongozi na wafuasi wa vyama vitano vya upinzani ikiwa ni pamoja na baadhi ya wafuasi wenye ushawishi mkubwa katika chama cha Cndd-Fdd wamekua wakijaribu kuingia mitaani ili kupinga nia ya rais Nkurunziza ya kugombea muhula watatu pamoja na kauli za vitisho zinazotolewa na vijana wa chama tawala cha Cndd-Fdd “Imbonerakure” dhidi ya wale wote wanaopinga kugombea kwa rais Nkurunziza muhula watatu.

Wakati huohuo idadi ya wakimbizi kutoka Burundi inaendelea kuongezeka katika nchi jirani. Alhamisi asubuhi wiki hii zaidi ya watu thelathini wamezuiliwa kwenye mpaka wa Burundi na Rwanda wakijaribu kukimbilia nchi Rwanda. Mpaka sasa Rwanda imewapokea wakimbizi wa Burundi zaidi ya 9,500. Shirika la Umoja wa Mataifa UNHCR limeanza zoezi la kuwahamisha wakimbizi hao kutoka katika makambi waliyokua walijengewa karibu na mpaka na Burundi, na watatengewa kambi kwenye umbali wa kilomiata 150 kama zinavyoeleza sheria za kimataifa zihusuzo wakimbizi.

Inasemekana kwamba raia wengine kutoka Burundi wamekua wakikimbilia Tanzania (kigoma na Ngara) pamoja na mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mkoa wa Kivu-Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.