Pata taarifa kuu
BURUNDI-USALAMA

Waandamanaji 600 washikiliwa na polisi Burundi,watatu wauawa katika mashambulizi

Watu watatu wameuawa ijumaa katika shambulizi la bomu lilolenga askari polisi nchini Burundi ambapo takribani watu mia sita wametiwa nguvuni wakati wa maandamano na ghasia za kupinga raisi wa taifa hilo kuwania muhula wa tatu wa uongozi.

Waandamaji nchini Burundi wanaopinga raisi wa taifa hilo kuwania ,muhula wa tatu wa uongozi
Waandamaji nchini Burundi wanaopinga raisi wa taifa hilo kuwania ,muhula wa tatu wa uongozi REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa Polisi nchini humo Generali Andre Ndayambaje aliliambia shirika la habari AFP kuwa maafisa wawili wa polisi waliuawa na mmoja kujeruhiwa katika wilaya ya Kamenge ya mji mkuu wa Bujumbura wakati raia wa kawaida akieleza kuwa kuna raia pia alipoteza maisha na wengine wawili kujeruhiwa.

Shambulizi kama hilo linatajwa kutekelezwa katikati mwa jiji hilo limejeruhi maafisa watatu ,mkuu huyo wa polisi amesema.

Afisa mmoja wa polisi ambaye aliomba jina lake lisitajwe ameeleza kuwa ni wazi kuwa waandamanaji walianzisha mashambulizi ya ghafla na kuongeza kuwa ikiwa wanataka vita wataipata.

Wadadisi wanaona kuwa huenda shambulizi hilo ni kazi ya waandamanaji lakini yaweza kuwa pia mbinu ya  maofisa kuelezea madai ya kuwa waandamaji wanatumia silaha.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.