Pata taarifa kuu
BURUNDI-Rennaissance-HAKI-SHERIA

Burundi : Innocent Muhozi asikilizwa na vyombo vya sheria

Nchini Burundi maandamano yameendelea leo Ijumaa katika wilaya mbalimbali za jiji la Bujumbura. Maandamano hayo yameendelea wakati ambapo mkurugenzi na mmiliki wa kituo cha redio na telivisheni Rennaissance Fm, Innocent Mohozi akisikilizwa kwenye Ofisi ya mashtaka.

Innocent Muhozi (kulia) akiondoka katika Ofisi ya mashtaka jijini Bujumbura, Burundi, Mei 22 mwaka 2015.
Innocent Muhozi (kulia) akiondoka katika Ofisi ya mashtaka jijini Bujumbura, Burundi, Mei 22 mwaka 2015. RFI/DT
Matangazo ya kibiashara

Rennaissance Fm ni moja ya vyombo vya habari binafsi vilivyoshambuliwa na kuchomwa moto wakati wa jaribio la mapinduzi, juma moja lililopita.

Innocent Muhozi amesikilizwa kwa muda wa masaa 4, lakini ameruhusiwa kurejea nyumbani kwake. Afisaa wa mashtaka amemsikiliza mkurugenzi huyo katika lengo la kuendesha uchunguzi kuhusu jaribio la mapinduzi.

Ofisi ya mashtaka imemuhoji mkurugenzi wa kituo cha redio na televisheni Rennaissance Fm kuhusu kurushwa hewani kwa tangazo la jenerali Godefroid Niyombare la mapinduzi ya serikali, Jumatano wiki iliyopita.

Mpaka hatua hii Innocent Muhozi ana imani kuwa hatorudi kufuatiliwa na vyombo vya sheria, lakini ana hofu kuwa huenda vyombo vya sheria vikashinikizwa kutumia mbinu nyingine ili awekwe jela.

“ Uchunguzi umeanzishwa, nina imani kuwa sintorudi kufuatiliwa, kwani tulitekeleza kazi yetu ya uandishi wa habari ”, amesema Innocent Muhozi.

Mpaka sasa Innocent Muhozi hajaikimbia nchi yake wala kuingia mafichoni kama wakurugenzi wa vituo vya redio binafsi vingine.

Mkurugenzi huyo wa kituo cha redio na runinga binafsi Rennaissance Fm ameeleza kuwa polisi ndio iliyovamia na kuchoma moto majengo ya kituo chake cha redio na runinga Rennaissance Fm.

Hayo yakijiri zaidi ya watu kumi na tano wamejeruhiwa katika maandamano ya leo Ijumaa.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.