Pata taarifa kuu
KENYA-AL SHABAB-MASHAMBULIZI-USALAMA

Kenya : makabiliano kati ya polisi na wanamgambo wa Al Shabab

Makabiliano makali kati ya vyombo vya usalama na wanamgambo wa Al Shabab yametokea Jumatatu usiku Mei 25, Kaskazini Magharibi mwa Kenya. Kijiji cha Yumbis na maeneo mengine yaliyopembezoni katika Kaunti ya Garissa, yamekua yakilengwa na wanamgambo hao wa Al Shabab.

Wanajeshi wa kenya kwenye eneo la shambulio, Garissa, Aprili 2 mwaka 2015.
Wanajeshi wa kenya kwenye eneo la shambulio, Garissa, Aprili 2 mwaka 2015. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Shambulio hilo limetokea usiku wa Jumatatu kuamkia Jumanne Mei 26 katika kijiji cha Yumbis, kwenye umbali wa kilomita zaidi ya hamsini Kaskazini Mashariki mwa Kaunti ya Garissa. Mashambulizi mawili yamefanyika kwa wakati mmoja.

Gari moja la polisi lililokua likipiga doria limekanyaga bomu lililotengenezwa kienyeji, na baadaye kulifuatiwa na urushianaji risasi. Muda mfupi baadaye msafara wa magari ya polisi yaliyotumwa kusaidia ili kuzima shambulio hilo, umeshambuliwa, na magari kadhaa yameharibiwa na wanamgambo hao wa Al Shabab.

Tangu Jumanne wiki hii, taarifa kutoka viongozi wa Kenya zimekua zikitafautiana. Msemaji wa polisi, George Kinoti, ametangaza mapema asubuhi kwamba makumi ya askari polisi walitoweka katika shambulio la kuvizia lililoendeshwa Jumatatu usiku wiki hii, huku akibaini kwamba operesheni ya kuwatafuta imeanzishwa.

Lakini tangazo la mkuu wa polisi, Joseph Boinett, leo Jumanne mchana limethibitisha kwamba kumekua na majeruhi na magari matano ya polisi yaliteketezwa kwa moto.

Wakati huo huo ikulu ya rais wa kenya kwenye mtandao wake wa kijamii, imetoa rambirambi zake kwa familia ziliyowakosa ndugu zao. Ujumbe huo uliyowekwa kwenye mtandao huo wa twitter ulifutwa, kabla ya waziri wa mambo ya ndani kutangaza kuwa askari polisi mmoja ameuawa na wengine wanne wamejeruhiwa. Waziri wa mambo ya ndani ametaja kuwa idadi ya askari polisi ishirini waliouawa inayotolewa na Al Shabab ni propaganda ya kundi hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.