Pata taarifa kuu

Kenya: yaadhimisha miaka 52 ya uhuru wake

Nchini ya Kenya inaadhimisha miaka 52 tangu ilipopata madaraka ya kujitawala kutoka kwa wakoloni kutoka Uingereza siku kama ya leo mwaka wa 1963.

Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto,Aprili 4 mwaka 2015 à Nairobi.
Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto,Aprili 4 mwaka 2015 à Nairobi. REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Maadhimisho ya mwaka huu yalihudhuriwa pia na rais wa Uganda Yoweri Museveni, Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa na wanasiada wa Sudan Kusini huku tishio la Al Shabab likizungumziwa katika maadhimisho hayo.

Maelfu ya watu walifurika katika uwanja wa michezo wa Nyayo jijini Nairobi kuadhimisha siku hii ambayo wakenya wanakumbuka kuanza safari ya kujikomboa kutoka kwenye minyororo ya wakoloni.

Maadhimisho ya mwaka huu yalihudhuriwa pia na rais wa Uganda Yower Museveni, Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramafosa na wanasiasa wanaozozana nchini Sudan Kusini.

Akiongoza maadhimisho hayo rais Uhuru Kenyatta amewasisitia wakenya kuendelea kuwa macho kutokana na vitisho vya kigaidi kutoka kundi la Al Shabab kutoka nchini Somalia na kuwaomba wazazi kutoa taarifa kwa polisi ikiwa kuna watoto wao waliotoweka katika mazingira ya kutatanisha wakati serikali ikihakikisha kuwa wananchi wanakuwa salama.

Akizungumza katika maadhimisho hayo , rais Yoweri Museveni amesema kundi la Al Shabab limeelemewa na wanajeshi wa Afrika na halina budi kusalimu amri.

Kuhusu mzozo wa Sudan Kusini, rais Kenyatta amesema viongozi wa kisiasa ambao wamekuwa wakiishi nchini Kenya kutokana na machafuko yanayoendelea katika taifa lao wanarudi nyumbani kuhimiza amani baada ya kupatana jijini Nairobi.

Naye Makamu wa rais wa Afrika Kusini Cyril Ramafosa aliyepata nafasi ya kuzungumza katika maadhimisho hayo ameiomba Kenya msamaha kutokana na raia wake kuvamiwa na wenyeji nchini mwake hivi karibuni.

Pamoja na kuwepo kwa wageni nje ya nchi, rais Kenyatta ameelezea mafanikio ya serikali yake na kuwaambia wakenya kushikamana na kuacha siasa za chuki zilizopigwa vita na waanzilishi wa taifa hilo zaidi ya miaka hamsini iliyopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.