Pata taarifa kuu
CHAD-MASHAMBULIZI-BOKO HARAM-USALAMA

Chad: washukiwa kadhaa watambuliwa

Siku mbili baada ya mashambulizi ya kujitoa mhanga Jumatatu wiki hii katika mji mkuu wa Chad, N'Djamena, na kusababisha vifo vya zaidi ya watu thelathini, uchunguzi umepelekea kukamatwa kwa washukiwa kadhaa.

Mashambulizi yalilenga kituo kikuu cha polisi, makao makuu ya Idara ya Usalama wa raia na chuo cha polisi, Juni 15.
Mashambulizi yalilenga kituo kikuu cha polisi, makao makuu ya Idara ya Usalama wa raia na chuo cha polisi, Juni 15. AFP PHOTO / BRAHIM ADJI
Matangazo ya kibiashara

Kunajulikana pia kuhusu utaratibu uliyotumiwa, wakati Chad ililinyooshea kidole hivi karibuni kundi la Boko Haram kuwa ndio lilihusika na mashambulizi hayo kutokana na mashambulizi inayoendesha dhidi ya kundi hilo la kiislamu.

Kwa sababu za usalama, serikali ya Chad pia imepiga marufuku kuvaa hijabu na kilemba.

Kamera za ulinzi zilipelekea kujua kuwa wahusika wa mashambulizi hayo kwenye kituo kikuu cha polisi pamoja na kwenye makao makuu ya Idara ya Usalama wa Raia hakuwa kwenye pikipiki bali kwa miguu. Pikipiki iliyopatikana katika eneo la tukio ni ya mtu ambaye alikuwa akitokea kwenye kituo cha polisi wakati wa mlipuko huo.

Picha ziliyopigwa na kamera za ulinzi zilipelekea watu wawili waliojilipua kutambuliwa. Wachunguzi wamebaini kuwa watu hao ni wakaazi wa jimbo la Ziwa karibu na Nigeria kutokana na utamaduni wao wa kujiweka makovu kwenye mwili. Wamiliki wa magari yaliyolipuka katika chuo cha polisi pia wametambuliwa. " Uchunguzi unaendelea vizuri", amesema mmoja kati ya wachunguzi.

Hata hivyo kama alivyotangaza rais wa Chad, Idriss Déby, jeshi la nchi hiyo liliendesha mashambulizi dhidi ya ngome za kundi la Boko Haram nchini Nigeria. Helikopta ziliendesha mashambulizi kwenye ngome sita za Boko Haram. Mpaka sasa hakuna kundi hata moja ambalo limekiri kuhusika na mashambulizi hayo ya N'djamena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.