Pata taarifa kuu
BURUNDI-EAC-USALAMA-SIASA

Mkutano wa marais wa (EAC) kuhusu mgogoro wa Burundi

Mkutano wa kilele wa tatu kuhusu mgogoro wa Burundi unafanyika leo Jumatatu jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania, kwa jitihada za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikutana jijini Dar es Salaam, Tanzania, Mei 31 mwaka 2015.
Marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakikutana jijini Dar es Salaam, Tanzania, Mei 31 mwaka 2015. .AFP PHOTO / STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Muhusika mkuu, rais Pierre Nkurunziza hatashiriki mkutano huu, kwani amedhamiria kuendelea na mpango wake wa kampeni za uchaguzi. Wenzake wa Ukanda huu wataendelea kwa mara nyingine kujaribu kupata ufumbuzi wa mgogoro unaoikabili Burundi wakati huu.

Mkutano wa awali wa marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, ambao ulifanyika mwezi mmoja uliyopita ulipendekeza mambo matatu kwa serikali ya Burundi: kuahirisha uchaguzi, kupokonya silaha wanamgambo na kuanzisha mazungumzo na upinzani.

Lakini yote hayo hayakufanyika na serikali imedhamiria kuendelea na mchakato wa uchaguzi. Uchaguzi wa wabunge na madiwani ulifanyika wiki Jumatatu Juni 29 na uchaguzi wa urais unatazamiwa kufanyika Julai 15. Ukosefu wa mazungumzo na zaidi ya yote vurugu ambazo zinaendelea. Kukataliwa kwa msuluhishi wa Umoja wa Mataifa Abdoulaye Bathily Jumapili Julaia 5 kunakuja kuzidisha utumiaji nguvu wa serikali kuendelea na uchaguzi, licha ya kupingwa kimataifa.

Wakati huo huo Spika wa Bunge la Burundi Pie Ntavyohanyuma na Makamu wa pili wa rais Gervais Rufyikiri wamewaandikia barua marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwataka kumuomba rais Pierre Nkurunziza kutothubutu kuwania muhula wa tatu, wakibaini kwamba ni kinyume na Katiba ya nchi na Mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha.

Pie Ntavyohanyuma na Gervais Rufyikiri wamebaini kwamba bado ni viongozi wa nchi ya Burundi, kwani hawajajiuzulu kwenye nyadhifa zao wala hakuna watu ambao wameshateuliwa kwenye nyadhifa zao.

Hali ya usalama imeendelea kudorora nchini Burundi, huku raia wakiendelea kuwa na hofu ya kutokea kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe.

Viongozi wa upinzani wamejielekeza nchini Tanzania ili kujaribu kuwashawishi marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki kuchukua hatua zinazohitajika dhidi ya rais Pierre Nkurunziza, ambaye hatashiriki mkutano huo wa marais, ambao unaaza leo jijini Dar es Salaam, nchini Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.