Pata taarifa kuu
MAREKANI-UINGEREZA-UN-SUDANI KUSINI-VIKWAZO

Marekani na Uingereza zaiomba UN kuchukulia vikwazo serikali ya sudan Kusini

Marekani na Uingereza zinaitaka Umoja wa Mataifa kuiwekea vikwazo serikali ya Sudan Kusini baada ya rais Salva Kiir kukataa kutia saini mkatba wa amani sik ya Jumatatu.

Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini  na mpinzani wake, hawakusiriki katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia.
Kiongozi wa waasi, Riek Machar (kulia) na rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir (kushoto) Mei 9 mwaka 2014. Lakini, rais wa Sudani Kusini na mpinzani wake, hawakusiriki katika mazungumzo ya amani, Addis Ababa, Ethiopia. REUTERS/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Mshauri wa maswala ya usalama wa rais Barrack Obama Bi Susan Rice amemshtumu rais Kiir kwa kushindwa kuonesha uongozni na kusema amepoteza nafasi ya kuleta amani katiam nchini yake.

Kiir ameahudi kurejea jijini Addis Ababa tarehe 2 mwezi ujao ili kutia saini mkataba huo baada ya kuoba siku 15 kwenda kushauriana na washirika wake.

Jumanne wiki hii Marekani iliitaka serikali ya Sudan Kusini kutia saini mkataba wa amani baada ya siku 15 kama ilivyoahidi ili kumaliza miezi 20 ya mapigano katika taifa hilo.
Mkataba huo ulitiwa saini Jumatatu wiki hii na kiongozi wa waasi Riek Machar huku rais Salva Kiir akiomba siku 15 kurudu nyumbani kwenda kushauriana na wenzake kabla ya kurejea tena jijini Addis Ababa kusaini mkataba huo.

John Kirby msemaji wizara ya mambo ya nje ya Marekani alisema Marekani imesikitishwa na hatua ya rais Kiir kutotia saini mkataba huo.

Msululishi wa mgororo huo Seyoum Mesfin  amasema kuwa licha ya serikali kutotia saini mkataba huo, hatua kubwa imepigwa kuelekea kupata amani.

Suala tata limekuwa ni namna ya kugawana madaraka kati ya Machar na Kiir na mkataba uliotiwa saini na Machar na Katibu mkuu wa chama cha SPLM Pagan Amum, unamrudisha Machar katika wadhifa wa Makamu wa rais wa nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.