Pata taarifa kuu
CAR-UN-TUHUMA-HAKI

CAR: askari 3 wa UN wakabiliwa na kesi tatu mpya za ubakaji

Askari watatu wa kulinda amani nchini jamhuri ya Afrika ya Kati wanahusishwa na kesi tatu mpya za ubakaji nchini humo. Taarifa hii ilitangazwa Jumatano wiki hii na msemaji wa Umoja wa Mataifa, wiki moja baada ya kuondolewa kwa mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo kwa makosa yanayofanana na hayo.

Askari wa kulinda amani katika mji wa Bangui, Oktoba 15, 2014.
Askari wa kulinda amani katika mji wa Bangui, Oktoba 15, 2014. AFP PHOTO / STRINGER
Matangazo ya kibiashara

Tuhuma hizi mapya za ubakaji wa wanawake watatu unaodaiwa kutekelezwa na askari hao watatu wa kikosi cha Minusca zimewekwa bayana na Vannina Maestracci, msemaji wa Umoja wa Mataifa, huku kukiwa na taarifa kuwa mmoja wa wanawake watatu waliobakwa ni binti mwenye umri mdogo mjini Bambari.

Madai hayo ya Ubakaji tayari yametolewa wiki chache zilizopita na kuripotiwa na familia za wahanga hao Agosti 12, kwa mujibu wa Bi Maestracci, bila ya kutoa uraia wa askari hao wa kulinda amani, licha ya kuwa askari pekee kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ndio wanaopatikana mjini Bambari, kaskazini mashariki mwa mji wa Bangui.

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wametoa wito kwa ajili ya mkutano wa dharura na wawakilishi wa DRC pamoja na kuitaarifu serikali ya nchi hiyo ili kuanza uchunguzi wa tuhuma hizo za kwanza baada ya kufutwa kazi kwa Mkuu wa minusca Babacar Gaye na za kwanza baada ya uteuzi wa Parfait Onanga-Anyanga.

Umoja wa Mataifa una jumla ya askari wa kulinda amani elfu 12 nchini Jamhuri ya Kati, kukiwa na jumla ya madai 61 ya Ubakaji na utovu wa nidhamu, ikiwa ni pamoja na madai 12 katika matukio ya unyanyasaji wa kijinsia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.