Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Joseph Kabila: “sijawahi kuomba marekebisho ya Katiba”

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amejibu kwa mara ya kwanza tangu mgawanyiko utokee ndani ya vyama vinavyomuunga mkono.

Joseph Kabila, Raiswa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo asema kuwa hajawahi kuomba Katiba ya nchi yake ibadilishwe.
Joseph Kabila, Raiswa jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo asema kuwa hajawahi kuomba Katiba ya nchi yake ibadilishwe. REUTERS/James Akena
Matangazo ya kibiashara

Katika mkutano uliofanyika siku ya Jumapili mwishoni mwa juma hili lililopita kwenye shamba lake la Kingakati, Rais Kabila amesema kuwa kamwe hajawai kuomba marekebisho yoyote ya Katiba, licha ya kuwa Rais huyo ameendelea kuibua hali ya sintofahamu kuhusu nia yake ya kugombea muhula wa tatu.

Wabunge 315 na maseneta 47 wameonyesha kumuunga mkono rais huyo na kuonyesha uaminifu wao kwake, amesema msemaji wa serikali Lambert Mende, na kumaliza mkutano wao bila ya kuwataja viongozi wa vyama 7 walioondoka katika muungano huo.

Rais Kabila amesisitizia umuhimu wa mazungumzo ya kitaifa ambayo yanataraiwa na wengi na kusema kuwa lazima muungano huo uwe tayari kukabiliana na uchaguzi ujao kwa vile kulingana naye, bado muungano huo una uwezo wa kushinda uchaguzi ujao.

Kabila amesema kuwa anashangaa kwa nini anaogopwa na kwa mujibu wa Lambert Mende, ambaye katika mahojiano na RFI amethibitisha kuwa ni wazi kwamba Rais huyo ataheshimu Katiba, huku Upinzani ukielezea wasiwasi wake na kuendelea kuomba Rais Kabila mwenyewe kujibu suala la kugombea kwake au la.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.