Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI-SIASA

Moïse Katumbi kusikilizwa kwa mara nyingine na Mwendesha mashitaka

Moïse Katumbi anatazamiwa kusikilizwa tena leo Jumatano na Mwendesha mashtaka mjini Lubumbashi katika mfumo wa uchunguzi kuhusu madai ya kuajiri askari mamluki wa kigeni.

Moise Katumbi aimarisha timu yake ya wanashria wa Congo kwa kumshirikisha mwanasheria kutoka Ufaransa Eric Dupond-Moretti.
Moise Katumbi aimarisha timu yake ya wanashria wa Congo kwa kumshirikisha mwanasheria kutoka Ufaransa Eric Dupond-Moretti. www.katanga.cd
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kuhojiwa kwa zaidi ya saa saba Jumatatu wiki hii, Moïse Katumbi ameamua kuimarisha utetezi wake, kwa kumshirikisha katika timu yake ya wanasheria wa Congo mwanasheria mashuhuri wa chama cha mawakili nchini Ufaransa: Wakili Eric Dupond-Moretti.

Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga na mgombea urais anatuhumiwa na mahakama ya nchi hiyo "kuajiri askari mamluki", hasa Wamarekani.

Mwanasheria wa masuala ya jinai kutoka Ufaransa, Eric Dupont-Moretti, amekubali kumtetea mpinzani wa DR Congo Moise Katumbi, Mei 10, 2016.
Mwanasheria wa masuala ya jinai kutoka Ufaransa, Eric Dupont-Moretti, amekubali kumtetea mpinzani wa DR Congo Moise Katumbi, Mei 10, 2016. © AFP/MEHDI FEDOUACH

"Mashirika ya kimataifa yanayotetea haki za binadamu yanasema kuwa kesi hii haieleweki, na kesi ya kisiasa yenye lengo tu kumzuia Moïse Katumbi kutowania katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwaka huu, " Bw Eric Dupond-Moretti ameiambia RFI. Ameongeza kuwa kuna uwezekano mkubwa wa "kusamfirisha mjini Kinshasa" mwanasiasa huyo wa upinzani wa Congo.

Wiki iliyopita, Moïse Katumbi alitangaza nia yake ya kuwania katika uchaguzi wa urais uliyopangwa kufanyika mwaka huu. Aliposikilizwa kwa mara ya kwanza Jumatatu wiki hii, Bw Katumbi alikana tuhuma dhidi yake.

Jumapili hii, Moïse Katumbi, kwenye akaunti yake ya twitter, ameiomba serikali iwajibike kwa usalama wa raia wa Jmhuri ya Kidemokrasia ya Congo badala ya kubuni kesi za uzushi dhidi yake.

"Serikali yetu inapaswa kuchukua hatua kuanzia sasa: kuongezeka juhudi za kijeshi, polisi na kisheria kwa kuhakikisha usalama umerejea nchini. Badala kubuni kesi bandia katika mji wa Lubumbashi, " amesema Bw Katumbi, huku akiwapongeza raia kumuunga mkono wakati alipokua akisikilizwa katika ofisi ya mashitaka mjini Lubumbashi Jumatatu wiki hii.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.