Pata taarifa kuu
GAMBIA-HAKI

Tume ya Ukweli na Maridhiano yawasilisha ripoti kuhusu uhalifu wa zama za Jammeh

Tume ya Ukweli, Maridhiano na Fidia imewaslisha tangu jana Alhamisi kwa Rais Adama Barrow ripoti kuhusu uhalifu uliotekelezwa katika utawala wa Yahya Jammeh.

Yahya Jammeh alipoondoka Gambia Januari 21, 2017.
Yahya Jammeh alipoondoka Gambia Januari 21, 2017. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii ni matunda ya zaidi ya miaka 2 ya kusikilizwa kwa waathiriwa, mashahidi na wahusika wa uhalifu uliofanywa chini ya utawala wa rais wa zamani Yahya Jammeh, ambaye yuko uhamishoni nchini Equatorial Guinea.

Katika mapendekezo yake, Tume inatoa wito wa kuchukuliwa hatua za kisheria dhidi ya wahusika wa uhalifu huu, bila hata hivyo kutoa maelezo zaidi.

Ni ripoti iliyosubiriwa kwa muda mrefu ambayo makamishna wa Tume ya Ukweli, Maridhiano na Fidia wameiwasilisha kwa rais Adama Barrow. Ripoti hiyo inapendekeza kwamba wale ambao kimsingi walihusika na uhalifu uliofanywa wakati wa utawala wa rais wa zamani Yahya Jammeh wafikishwe mahakamani, amesema Mwenyekiti wa Tume Lamin Sise.

"Katika ripoti yake, Tume imetambua na kupendekeza kufunguliwa mashtaka kwa wale waliohusika zaidi na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu na unyanyasaji uliofanywa dhidi ya Wagambia na wasio Wagambia kati ya mwezi wa Julai 1994 na Januari 2017."

Moja ya maswali makubwa yanahusiana na mapendekezo yaliyomo katika ripoti hii. Hasa juu ya hitaji au la ambapo rais wa zamani - ambaye sasa yuko uhamishoni nchini Equatorial Guinea - aliwajibika.

Kwa vyovyote vile, mkuu wa nchi Adama Barrow ametaka kuwahakikishia nia yake ya kuona mchakato huo ukikamilika. “Nawahakikishia, serikali yangu itaichunguza ripoti hiyo kwa makini, ili kuchukua hatua stahiki. Kisha serikali itafahamisha umma kuhusu msimamo wake itakaotangaza miezi sita kuanzia leo. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.