Pata taarifa kuu

Mwili wa Rais wa zamani wa Angola José Eduardo Dos Santos yawasili Luanda

Familia ya rais wa zamani wa Angola aliye kuwa madarakani kwa takriban miaka 40 na ambaye alifariki nchini Uhispania mwezi uliopita inakinzana kuhusiana na mazishi ambayo yatafanyika katika mji mkuu wa Angola.

Jeneza la aliyekuwa rais wa Angola, Dos Santos, aliyefariki nchini Uhispania mwezi Julai, likishushwa kutoka kwenye ndege, mjini Luanda, Agosti 20, 2022.
Jeneza la aliyekuwa rais wa Angola, Dos Santos, aliyefariki nchini Uhispania mwezi Julai, likishushwa kutoka kwenye ndege, mjini Luanda, Agosti 20, 2022. © REUTERS - SIPHIWE SIBEKO
Matangazo ya kibiashara

Ndege kutoka Barcelona, ​​​​nchini Uhispania, ikiwa na mwili wa rais wa zamani ilitua katika mji mkuu wa Angola Jumamosi jioni, waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP wamebaini. Watu 20 walikuwepo kwenye uwanja wa ndege kupokea jeneza la José Eduardo Dos Santos. Watoto kadhaa wa hayati rais na mjane wake Ana Paula Dos Santos pia walikuwepo. Wafuasi wake walipiga makofi wakati jeneza lililokuwa na bendera ya Angola likipita.

Baada ya miezi kadhaa ya vita vya kisheria nchini Uhispania, hatimaye Ana Paula Dos Santos alitumia uamuzi wa Mahakama ya Juu ya Haki ya Catalonia, ambayo ilimkabidhi mwili wa mume wake, kumrudisha haraka iwezekanavyo nchini Angola.

Paula Dos Santos alikabilina na upinzani mkali kutoka kwa binti-mkwe wake, Tchizé Dos Santos. Alitaka mazishi yafanyike nchini Uhispania kwa sababu anamshutumu rais wa sasa kwa kurejesha sura ya babake ili kuendeleza kuchaguliwa kwake tena. Miezi michache iliyopita alipoingia kwenye kampeni, João Lourenço, ambaye anaongoza nchi hiyo tangu 2017, alitoa wito wa kupigiwa kura "kuheshimu kumbukumbu" ya hayati rais. "Aibu kuwa" amesema Tchizé Dos Santos ambaye anamshutumu João Lourenço kwa ufisadi na ubadhirifu wa fedha za umma dhidi ya familia yake.

Lakini rufaa iliyowasilishwa kwa mahakama ya Uhispania haikuzuia kusafirishwa kwa mwili wake nchini Angola. 

Jose Eduardo dos Santos, ambaye aliiongoza Angola bila kupingwa kuanzia 1979 hadi 2017, alifariki Julai 8, akiwa na umri wa miaka 79, katika kliniki moja huko Barcelona alikokuwa amelazwa hospitalini baada ya kupata mshtuko wa moyo mnamo Juni 23.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.