Pata taarifa kuu

Wasiwasi watanda katika mji wa Goma na viunga vyake kufuatia mapigano kati ya FARDC na M23

Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya jitihada za kidiplomasia, mapigano kati ya waasi wa M23 na wanajeshi wa serilkali yameendelea, ripoti zikieleza kuwa waasi hao wako umbali wa Kilomita 20 kutoka mjini Goma. 

Wanajeshi wa jeshi la Kongo wakishika doria katika eneo la Kanyaruchinya ambako watu walilitoroka makazi yao kufuatia kusonga mbele kwa M23.
Wanajeshi wa jeshi la Kongo wakishika doria katika eneo la Kanyaruchinya ambako watu walilitoroka makazi yao kufuatia kusonga mbele kwa M23. REUTERS - ARLETTE BASHIZI
Matangazo ya kibiashara

Mapigano haya yameendelea kuwapa wasiwasi, wakaazi wa Goma na maeneo jirani, huku jeshi likiwahakikishia raia kuwa, limewadhibiti waasi wa M23 huko Kibumba. 

Jenarali Constant Ndima ni Gavana wa Kijeshi katika jimbo la Kivu Kaskazini. 

Hakikisho hili linakuja baada ya hapo jana mchana uvumi kusambaa kuwa waasi wa M23 walikuwa wanakaribia Goma, huku wakazi wakisema waliwaona baadhi ya wanajeshi wa serikali kwenye pikipiki wakiondoka kwenye mji huo. 

Msuluhishi wa mzozo huu kutoka nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta, aliyezuru Goma jana, aliwatembelea wakimbizi katika kambi ya  Kanyaruchinya na kushuhudia masaibu yao. 

Tangu waasi wa M23 kusonga mbele katika makabiliano yao na jeshi la DRC, hali hii imesababisha maelfu ya watu kuyakimbia makwao. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.