Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi Equatorial Guinea: Teodoro Obiang Nguema ashinda uchaguzi kwa muhula wa sita

Rais wa Equatorial Guinea Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ambaye tayari ametumia miaka 43 madarakani, ameshinda uchaguzi wa urais wa Novemba 20 kwa zaidi ya 94% ya kura.

Obiang, mwenye umri wa miaka 80, aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi ya jeshi ya mnamo mwaka 1979. Hivi sasa Nguema ndiye kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi ukiondoa orodha ya watawala wa kifalme.
Obiang, mwenye umri wa miaka 80, aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi ya jeshi ya mnamo mwaka 1979. Hivi sasa Nguema ndiye kiongozi aliyekaa madarakani kwa muda mrefu zaidi ukiondoa orodha ya watawala wa kifalme. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Kulingana na matokeo yaliyosomwa kwenye televisheni ya umma na Faustino Ndong Esono Eyang, Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye pia ni mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi, waliojitokeza kwa kupiga kura walikuwa 98%.

Rais Obiang Nguema, mgombea kwa muhula wa sita mfululizo, alipata 94.9% ya kura kati ya zaidi ya wapiga kura 413,000. Mpinzani wake mkuu, Andrès Esono Ondo, alipata kura 9,684 pekee, sawa na  takriban 4% ya kura.

Upinzani bila ya kuwa na kiti bungeni

Kuhusu uchaguzi wa wabunge, Chama cha Kidemokrasia cha Equatorial Guinea (PDGE) cha Rais Obiang Nguema na vyama washirika 14 vimeshinda viti vyote 100 katika Bunge la kitaifa.

Ushind kama huo pia umeripotiwa katika Bunge la Seneti ambapo viti 55 pia viko chini ya udhibiti wa mamlaka. Lakini kwa vile Bunge hili linapaswa kuwa na wajumbe 70, hao wengine 15 watateuliwa na Rais wa Jamhuri kwa mujibu wa Katiba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.