Pata taarifa kuu

Equatorial Guinea: Mtoto wa kiume wa Rais Obiang akamatwa kwa madai ya ufisadi

Mmoja wa watoto wa kiume wa rais wa Equatorial Guinea, Ruslan Obiang Nsue, anayeshukiwa kuuza ndege kutoka shirika la ndege la kitaifa, alikamatwa Jumatatu na kuwekwa chini ya kizuizi cha nyumbani, televisheni ya serikali (TVGE) imetangaza Jumanne hii Januari 17.

Equatorial Guinea imetawaliwa kwa zaidi ya miaka 43 na Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ambaye ndio kwanza amechaguliwa tena kwa muhula wa sita wa miaka saba na anashikilia rekodi ya dunia ya kukaa muda mrefu madarakani kwa mkuu wa nchi aliye hai, bila kujumuisha wafalme.
Equatorial Guinea imetawaliwa kwa zaidi ya miaka 43 na Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ambaye ndio kwanza amechaguliwa tena kwa muhula wa sita wa miaka saba na anashikilia rekodi ya dunia ya kukaa muda mrefu madarakani kwa mkuu wa nchi aliye hai, bila kujumuisha wafalme. AFP - SAMUEL OBIANG
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa mwezi Novemba, mamlaka ilifungua uchunguzi "baada ya kubainika kutoweka kwa ndege ya ATR 72-500 mali ya kampuni ya kitaifa", Ceiba Intercontinental, ambayo ilikuwa katika ukarabati wa kawaida nchini Uhispania tangu 2018, TVGE imeripoti.

Kulingana na chanzo hicho, Bw. Obiang Nsue, aliweza "kuuza ndege ya ATR kwa kampuni ya Binter Technic", iliyobobea katika matengenezo ya ndege na yenye makao yake Las Palmas, kwenye kisiwa cha Uhispania cha Gran Canaria. Aliyekuwa Katibu waziri wa Michezo na Vijana, Ruslan Obiang Nsue, mkurugenzi wa sasa wa Uwanja wa Ndege wa Ceiba, kwanza alikuwa naibu mkurugenzi wa Ceiba Intercontinental na kisha meneja wake mkuu.

“Ruslan Obiang alikiri kuwa yeye ndiye aliyeuza ATR ya Ceiba, sitaingiliwa na ukabila au upendeleo, ndiyo maana nimeamuru akamatwe mara moja na kuwekwa mbele ya vyombo vya sheria,” kaka yake wa kambo, Makamu wa Rais Teodoro Nguema Obiang Mangue, aliyepewa jina la utani "Teodorin," ameandika kwenye ukurasa wake wa Twitter.

Teodorin Obiang mwenyewe alihukumiwa na mahakama ya Ufaransa mwishoni mwa mwezi Julai 2021 kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya euro milioni 30 na kutaifisha mali yake nchini Ufaransa kwa kuanzisha biashara ya kifahari nchini humo kwa njia ya udanganyifu katika muktadha wa kesi za "manufaa yaliyopatikana kwa njia mbaya".

Mnamo mwezi Julai 2021, London pia ilizuia mali yake ya kifedha nchini Uingereza na kumpiga marufuku nchini humo kufuatia uchunguzi dhidi ya ufisadi. Malabo kisha ailifunga ubalozi wake nchini Uingereza kupinga uamuzi huu.

Kukamatwa kwa Ruslan Obiang Nsue, mmoja wa watoto wa kiume wa rais, ni jambo lisilo na kifani kwa mwanachama wa familia ya rais wa taifa hili dogo la Afrika ya Kati lenye utajiri wa mafuta. Mwezi Desemba mwaka uliyopita, habari za kutoweka kwa ndege hii na kudhaniwa kuuzwa kwake na Bw. Obiang Nsue ziliibua hasira nchini.

Equatorial Guinea imetawaliwa kwa zaidi ya miaka 43 na Rais Teodoro Obiang Nguema Mbasogo, ambaye ndio kwanza amechaguliwa tena kwa muhula wa sita wa miaka saba na anashikilia rekodi ya dunia ya kukaa muda mrefu madarakani kwa mkuu wa nchi aliye hai, bila kujumuisha wafalme. Equatorial Guinea ni nchi ya tatu kwa utajiri katika eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara kwa Pato la Taifa kwa kila mtu mwaka 2021 kulingana na Benki ya Dunia, lakini iliorodheshwa ya 172 duniani kati ya 180 katika kipimo cha rushwa cha shirika la kimataifa la Transparency International.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.