Pata taarifa kuu
UCHAGUZI-SIASA

Chama cha Rais chashinda viti vyote katika Bunge la Seneti nchini Cameroon

Chama cha Rais Paul Biya, ambaye anatawala nchini Cameroon bila kugawana madaraka kwa zaidi ya miaka 40, kimeshinda bila mshangao wowote viti vyote 70 katika Bunge la Seneti katika uchaguzi uliyofanyika Machi 12, Baraza la Katiba limetangaza.

Paul Biya anatawala Cameroon tangu 1982 kwa mkono wa chuma.
Paul Biya anatawala Cameroon tangu 1982 kwa mkono wa chuma. Ludovic MARIN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Rais Paul  Biya, 90, pia atateua ndani ya siku 10 zijazo maseneta zaidi 30. Chama cha DRPC kimeimarisha utawala wake wote katika Bunge la Seneti kwani upinzani ulikuwa na viti saba katika Bunge la Seneti linalomaliza muda wake.

Chama cha  RDPC kimeshinda viti vyote katika kila moja ya mikoa, kulingana na matokeo yaliyosomwa na Clément Atangana, Rais wa Baraza la Katiba, wakati wa hafla iliyoruswa hewani moja kwa moja kwenye televisheni ya serikali, CRTV.

Katika mikoa kumi ya nchi hii ya Afrika ya Katiyenye wakazi milioni 28, vyama 10 viliwasilisha wagombea kwa wapiga kura 11,134: madiwani wa mkoa, madiwani wa manispaa na viongozi wa jadi.

RDPC kilikuwa chama pekee kuwa na orodha katika mikoa yote kumi. Kinadhibiti manispaa 316 kati ya 360 nchini Cameroon. Katika Bunge la Kitaifa, Chama cha Bw. Biya na washirika wake pia wana idadi kubwa ya wabunge 164 kati ya 180, waliochaguliwa mnamo mwezi Februari 2020.

Paul Biya anaongoza Cameroon tangu 1982 kwa mkono wa chuma, ambaye anashtumiwa mara kwa mara na Umoja wa Mataifa pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali ya kimataifa kukandamiza upinzani na waasi wanaotaka mikoa yao kujittawala katika mikoa miwili ya Magharibi inayozungumza Kiingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.