Pata taarifa kuu

Guinea: Tisa wafariki katika shambulio dhidi ya gereza la Conakry siku ya Jumamosi

Takriban watu tisa waliuawa siku ya Jumamosi mjini Conakry katika operesheni ya kundi la watu waliokuwa wamejihami kwa silaha nzito ambao waliwatorosha kwa muda dikteta wa zamani Moussa Dadis Camara na wafungwa wenzake watatu kutoka gerezani, ofisi ya mwendesha mashtaka mkuu imesema siku ya Jumatatu asubuhi.

Moussa Dadis Camara, kiongozi wa Guinea wakati wa mauaji ya Septemba 28, 2009 huko Conakry, akizungumza mahakamani wakati wa kesi yake Septemba 28, Desemba 12, 2022.
Moussa Dadis Camara, kiongozi wa Guinea wakati wa mauaji ya Septemba 28, 2009 huko Conakry, akizungumza mahakamani wakati wa kesi yake Septemba 28, Desemba 12, 2022. © LAMARANA DJEBOU SOW / AFPTV
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa vifo hivyo ni washambuliaji watatu, maafisa wanne wa pilisi na watu wawili waliokuwa ndani ya gari la wagonjwa, ambao inaonekana ni raia wa kawaida, kulingana na ripoti ya muda iliyotolewa kwenye taarifa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali Yamoussa Conte.

Vyombo vya habari viliripoti kwamba raia walipigwa risasi wakiwa ndani ya gari la wagonjwa mahututi katika ubadilishanaji risasi kati ya washambuliaji na vikosi vya usalama.

Kundi la watu waliokuwa wamejihami kwa siklaha nzito walishambulia gereza kuu katikati mwa mji mkuu mapema Jumamosi na kuwatorosha kiongozi wa zamani wa mapinduzi Moussa Dadis Camara na wafungwa wengine watatu, wote wanne ambao kwa sasa wanashitakiwa kwa mauaji yaliyofanywa mwaka 2009 chini ya utawala wake.

Watatu kati yao, akiwemo Kapteni Dadis Camara, walikamatwa na kurejeshwa jela siku hiyo hiyo, bila ya kuwa wazi kama walitoroka au kuchukuliwa kinyume na matakwa yao, kama mawakili wao wanavyosema. Mtu wa nne, Claude Pivi, ambaye pia ni miongoni mwa washitakiwa wakuu katika kesi hiyo, bado anasakwa.

Mwanasheria Mkuu wa serikali amesema katika taarifa yake kwamba almeanzisha kesi dhidi ya Moussa Dadis Camara na wafungwa wenzake watatu kwa mauaji ya wanachama wa vikosi vya usalama na kuua bila kukusudia.

Moussa Dadis Camara na maafisa kumi wa kijeshi na serikali wamekuwa wakijibu tangu Septemba 2022 mahakamani kwa mlolongo wa mauaji, vitendo vya utesaji, ubakaji na utekaji nyara mwingine uliofanyika Septemba 28, 2009 na siku zilizofuata na vikosi vya usalama katika uwanja wa michezo wa kitongoji cha Conakry, ambapo makumi ya maelfu ya wafuasi wa upinzani walikusanyika, na maeneo jirani.

Takriban watu 156 waliuawa na mamia kujeruhiwa, na wanawake wasiopungua 109 kubakwa, kulingana na ripoti ya tume ya uchunguzi iliyopewa mamlaka na Umoja wa Mataifa.

Utawala wa kijeshi ulichukua mamlaka kwa nguvu mnamo mwezi Septemba 2021 ulichapisha mfululizo wa nakala Jumapili jioni ukitangaza kufutwa kazi kwa askari kadhaa na maafisa wa mamlaka wa magereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.