Pata taarifa kuu

Sierra Leone: Milio ya risasi yasikika Freetown, hali ya wasiwasi yatanda

Sierra Leone, nchi ya Afrika Magharibi, kwa sasa iko chini ya amri ya kutotoka nje, baada ya tukio la kurushiana risasi, katika mji mkuu, Freetown, tangu asubuhi ya Jumapili, Novemba 26.

Muonekano wa Freetown kutoka Signal hill.
Muonekano wa Freetown kutoka Signal hill. (V.Cagnolari)
Matangazo ya kibiashara

 

Na mwanahabari wetu mjini Freetown, Kadiatou Diallon, kutoka timu ya wahariri ya RFI Fulfulde

Wakaazi wa Freetown waliamshwa Jumapili hii asubuhi na milio ya risasi ya hapa na pale, na kuwalazimisha kujificha majumbani mwao.

Shughuli za usafiri katika mji mkuu zimepigwa marufuku na polisi ambayo imefunga mitaa kadhaa kuzuia njia yoyote na mikusanyiko.

Katika masoko, maduka madogo na makubwa yamefungwa. Kuna wachuuzi wachache tu wa mitaani.

Gereza Kuu la Pademba Road pia limevamiwa na wafungwa kuachiwa. Miongoni mwao, mwimbaji Boss Lee ambaye alifungwa katika moja ya magereza makubwa nchini kwa matusi.

Usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili, Novemba 26, ghala la silaha la Wilberforce lilivamiwa na watu ambao bado hawajajulikana ambao walichukua silaha na risasi.

Sheria ya kutotoka nje imewekwa na wakaazi wanaombwa kusalia nyumbani, kulingana na taarifa kutoka kwa Waziri wa Habari.

Kwa miaka kadhaa, wananchi wa Sierra Leone wamekuwa wakikabiliwa na mzozo wa kiuchumi ambao haujawahi kushuhudiwa ambao ulisababisha ghasia za wananchi mwaka 2022. Wakati huo, kulikuwa na wahanga 30, wakiwemo raia na wanajeshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.