Pata taarifa kuu

Sierra Leone: Serikali inasema inadhibiti hali ya mambo baada ya tukio la urushianaji riasasi

Serikali ya Sierra Leone imehakikisha kwamba vikosi vya usalama vimewarudisha kwenye viunga vya Freetown wale waliohusika na mapigano ambayo yametikisa mji mkuu tangu Jumapili asubuhi, na kwamba "inadhibiti" hali ya mambo.

Makabiliano ya kijeshi yametikisa mji mkuu wa Sierra Leone Freetown Jumapili asubuhi baada ya kushindwa kwa jaribio la kuvunja ghala la silaha, kulingana na serikali, ambayo imetangaza sheria ya kutotoka nje.
Makabiliano ya kijeshi yametikisa mji mkuu wa Sierra Leone Freetown Jumapili asubuhi baada ya kushindwa kwa jaribio la kuvunja ghala la silaha, kulingana na serikali, ambayo imetangaza sheria ya kutotoka nje. © REUTERS
Matangazo ya kibiashara

"Serikali inaendelea kudhibiti na inadhibiti hali ya mambo," Wizara ya Habari imesema katika taarifa iliyorushwa kwenye mitandao ya kijamii. Wizara hiyo imekiri kwamba "washambuliaji" walishambulia magereza ya Freetown na kwamba wafungwa wengi walitoroka, bila maelezo zaidi kuhusu "washambuliaji" hawa.

Mapigano makali yalitikisa mji mkuu wa Sierra Leone Freetown Jumapili asubuhi baada ya kushindwa kwa jaribio la kuvunja ghala la silaha za jeshi, kulingana na serikali, ambayo imetangaza sheria ya kutotoka nje.

Video zilizorushwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha kuwa wafungwa wengi walitoroka kutoka katika gereza kuu, katika mazingira ambayo bado haijathibitishwa. Mwanamume mmoja ambaye alikuwa sehemu ya kundi lililorekodiwa barabarani na mwandishi wa shirika la habari la AFP alibaini kwamba yeye na wengine walikuwa wafungwa waliotoroka.

Hali ilikuwa ya sintofahamu katikati ya mchana, huku viongozi wakiwa kimya baada ya kuhakikisha kuwa walidhibiti hali ya mambo mapema asubuhi.

Asili ya matukio bado haijulikani.

Mamalaka imetaja tu shambulio la ghala la silaha. Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Afrika Magharibi (ECOWAS) ilizungumza katika taarifa yake kwa vyombo vya habari kuhusu jaribio la kupata silaha, lakini pia "kuvuruga amani na utaratibu wa kikatiba", lugha inayotumiwa sana kufanya mapinduzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.