Pata taarifa kuu

Sierra Leone: Wengi wa waliohusika na shambulio la kambi wakamatwa, rais atangaza

Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio amesema hivi punde Jumapili usiku kwamba utulivu umerejea baada ya siku moja ya makabiliano ya kijeshi mjini Freetown ambayo ameyachukilia kama jaribio la kuhatarisha usalama wataifa na ambapo wengi wa waliohusika wamekamatwa kulingana na rais wa Sierra Leone.

Watu wamelazimika kusalia majumbani kwao huko Freetown, mji mkuu wa Sierra Leone, Jumapili hii, Novemba 26, 2023.
Watu wamelazimika kusalia majumbani kwao huko Freetown, mji mkuu wa Sierra Leone, Jumapili hii, Novemba 26, 2023. AP - TJ Bade
Matangazo ya kibiashara

"Utulivu umerejea," rais amehakikisha wakati wa hotuba fupi kwenye runinga ya serikali, baada ya kile alichoelezea kama "jaribio la kuyumbisha amani na utulivu ambao tunajaribu kufanyia kazi kwa bidii." "Viongozi wengi wamekamatwa" na itabidi wawajibishwe, amesema Julius Maada Bio, baada ya washambuliaji wasiojulikana walipojaribu kuvunja ghala la silaha huko Freetown, wakipambana na vikosi vya usalama katika maeneo kadhaa ya mji mkuu na kuwatorosha wafungwa wengi.

Waziri wa Habari Chernor Bah hapo awali alitangaza kwamba "hali ya usalama huko Freetown (ilikuwa) chini ya udhibiti thabiti wa serikali". Alikiri kwamba "washambuliaji" walishambulia magereza ya Freetown na kwamba wafungwa wengi walitoroka, bila maelezo zaidi juu ya "washambuliaji" hawa.

Hali ya utulivu imerejea jijini, amebainisha mwandishi wa shirika la habari la AFP. Hata hivyo, vituo vya ukaguzi vinavyolindwa na vikosi vikubwa vya usalama viliendelea kuwepo.

Wizara ya Habari inaeleza kuwa kwa sasa takwimu zinakusanywa ili kufanya tathmini na kutangaza idadi ya waliokamatwa.

Video zilizochapishwa kwenye mitandao ya kijamii zinaonyesha wanaume wachache waliovalia sare wakionekana kukamatwa wakiwa nyuma au karibu na gari la kijeshi. Mitandao ya kijamii imetaja, pamoja na ushahidi wa picha, aliyekuwa mlinzi wa rais wa zamani Ernest Bai Koroma (2007-2018) kama mmoja wa washiriki katika operesheni iliyotibuliwa na vikosi vya usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.