Pata taarifa kuu
MAPINDUZI-USALAMA

Sierra Leone: Rais ahutubia taifa wiki moja baada ya jaribio la mapinduzi

Rais wa Sierra Leone Julius Maada Bio amelihutubia taifaJumamosi usiku akitoa tena wito wa umoja, huku akitoa maneneo makali kwa wale ambao walitaka kuangusha taasisi zilizochaguliwa kidemokrasia.

Baada ya jaribio la mapinduzi, Rais Julius Maada Bio ametoa tena wito wa umoja, huku akiwakemea vikali wale ambao walitaka kushambulia taasisi zilizochaguliwa kidemokrasia.
Baada ya jaribio la mapinduzi, Rais Julius Maada Bio ametoa tena wito wa umoja, huku akiwakemea vikali wale ambao walitaka kushambulia taasisi zilizochaguliwa kidemokrasia. REUTERS - PHIL NOBLE
Matangazo ya kibiashara

Mnamo Novemba 26, kundi la watu wasiojulikana walishambulia kambi za kijeshi, ghala la silaha na vituo wanakozuilia wahalifu, pamoja na gereza kuu. Mapigano yalizuka na jeshi, na kusababisha vifo vya watu 21, wakiwemo wanajeshi 14 na washambuliaji 3. Watu 14 walikamatwa na zaidi ya thelathini wanatafutwa. Zaidi ya wafungwa 2,000 pia walifanikiwa kutoroka. Jaribio la kuvuruga utulivu lilifanywa kwa mujibu wa mamlaka na askari wakishirikiana na askari waliostaafu, miezi michache tu baada ya uchaguzi wa mwezi wa Agosti mwaka huu.

"Kitendo chao kilipangwa, kiliratibiwa na kutekelezwa ili kuondoa serikali iliyochaguliwa kidemokrasia, kupindua utawala wa kikatiba, na kuharibu miongo yetu ya uwekezaji katika amani na demokrasia. Walikamatwa na uchunguzi kuanzishwa. Polisi wametoa orodha ya watu wanaosakwa.” Julius Maada Bio kwa hivyo "kwa nguvu" anahimiza raia kutoa "taarifa yoyote muhimu ambayo itawezesha watu hao kukamatwa na kusaidia katika uchunguzi. "

"Jaribio hili la mapinduzi ambalo hutokea miezi mitano baada ya uchaguzi, kujaribu kupindua matakwa ya watu, ni dhambi kubwa na isiyoweza kusameheka," amesema rais. Kwa wale ambao walitaka kuvuruga demokrasia yetu: hawatafanikiwa! Vyovyote uchochezi, mwitikio wetu kwa matukio ya tarehe 26 utapimwa na kuamuliwa kwa kigezo kimoja: utawala wa sheria. Jaribio la mapinduzi kwa hiyo litachukuliwa kama tatizo la sheria na utaratibu pekee. Si suala la kisiasa, kikabila au kidini. "

Rais wa Sierra Leone hatimaye ametoa wito kwa raia kupinga mabadiliko yoyote kinyume na katiba, "shambulio lolote juu ya amani yetu, usalama wetu na demokrasia yetu", na kusema "hapana" kwa mtu yeyote au kwa kundi lolote "litachagua kuweka maslahi yake binafsi" juu ya maslahi ya taifa. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.