Pata taarifa kuu

Uchaguzi nchini DRC: Utata mpya waibuka juu ya uraia wa Moïse Katumbi

Kampeni za uchaguzi mkuu wa Desemba 20, 2023 zinaendelea kikamilifu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Chini ya wiki mbili kabla ya uchaguzi, utata kuhusu uraia wa mmoja wa wagombea urais, Moïse Katumbi, umeibuka tena. 

Moïse Katumbi wakati wa mkutano wake huko Goma katika kampeni za uchaguzi wa urais, mashariki mwa DRC, Novemba 23, 2023.
Moïse Katumbi wakati wa mkutano wake huko Goma katika kampeni za uchaguzi wa urais, mashariki mwa DRC, Novemba 23, 2023. AFP - ALEXIS HUGUET
Matangazo ya kibiashara

Zimesalia wiki mbili kabla ya uchaguzi mkuu uliopangwa kufanyika tarehe 20 Desemba 2023 nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC): uchaguzi wa urais, uchaguzi wa wabunge, uchaguzi wa magavana na uchaguzi mdogio wa serikali za mitaa.

Nchi inamaliza wiki yake ya tatu ya kampeni. Kuhusu uchaguzi wa urais, wagombea kadhaa wanazunguka nchi nzima kwa mikutano ya kuwatafuta watakao wapigia kura.

Mara kadhaa

Kando ya kampeni hii, utata umeibuka tena: unahusu uraia wa Moïse Katumbi, anayeonekana kama mmoja wa wapinzani wakuu kwa rais anayemaliza muda wake na mgombea wa muhula mpya, Félix Tshisekedi.

Mzozo huu mpya umeibuka kwa hatua kadhaa. Kwanza kabisa, wakati wa mkutano huko Lubumbashi katika mkoa wa Katanga, Rais Félix Tshisekedi aliwakashifu wagombea hawa ambao "watakuja hapa, na kujieleza kwa Kiswahili", lugha inayozungumzwa katika nchi kadhaa barani ikiwa ni pamoja na DRC. Dokezo hasa kwa Moïse Katumbi. Rais ambaye alitoa hotuba yake kwa Lingala - lugha nyingine inayozungumzwa nchini Kongo na nchi nyingine jirani - katika jimbo ambalo wazungumzaji wa Kiswahili ni wengi.

Lakini shambulio la moja kwa moja lilitoka kwa Jean-Pierre Bemba, Waziri wa Ulinzi na Naibu Waziri Mkuu, ambaye anafanya kampeni kwa niaba ya mkuu wa nchi anayemaliza muda wake. Wakati huu akiwa Kinshasa, alipinga moja kwa moja mgombea husika: "Ninatuma ujumbe kwa Moïse Katumbi, kwamba aje kuwaambia watu wa Kongo kama yeye ni Mzambia au la. Hatuwezi kutumikia mabwana wawili kwenye ngazi ya juu serikalini. Utaishia kumsaliti mmoja kwa faida ya mwingine. "

Shambulio ambalo lilisukuma kambi ya wapinzani kujibu, hasa kwa kusambaza hati kutoka kwa mamlaka ya Zambia ya Julai 11 na kujibu ombi la mawakili wa Katumbi. Barua hii, iliyotiwa saini na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Zambia, inasema mgombea huyo hana uraia wa Zambia. Barua hii ilikuwa imeombwa na ukoo wa Katumbi ili kukabiliana na uwezekano wa kugombea urais katika Mahakama ya Kikatiba. Uchunguzi ambao kwa hakika ulitolewa na mgombea mwingine, Noël Tshiani. Na Mahakama ya DRC iliamua swali hili mwezi Oktoba: ilihukumu ombi hilo lililokubaliwa kwa fomu, lakini lisilo na msingi wowote na hivyo kuthibitisha uraia wa Kongo wa Moïse Katumbi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.