Pata taarifa kuu

Rais wa Namibia Hage Geingob, mwanaharakati dhidi ya ubaguzi wa rangi, afariki dunia

Rais wa Namibia, Hage Geingob, amefariki leo Jumapili akiwa na umri wa miaka 82, ofisi ya rais imtangaza katika ujumbe uliochapishwa kwenye mtandao wa kijamii X. Alikuwa kiongozi na mtetezi wa uhuru na mpinzani mkubwa wa utawala wa kibaguzi.

Rais wa Namibia Hage Geingob katika Mkutano Mkuu wa 72 wa Umoja wa Mataifa mjini New York Septemba 20, 2017.
Rais wa Namibia Hage Geingob katika Mkutano Mkuu wa 72 wa Umoja wa Mataifa mjini New York Septemba 20, 2017. ©Jewel SAMAD/AFP
Matangazo ya kibiashara

 

Rais wa Namibia, Hage Geingob, aliyekuwa mtetezi wa uhuru na mpinzani mkubwa wa utawala wa kibaguzi, amefariki mapema Jumapili Februari 4 akiwa na umri wa miaka 82 hospitalini alikokuwa akitibiwa saratani, ofisi ya rais imetangaza.

Hage Geingob, aliyechaguliwa kuwa rais mwaka 2014, alifariki dunia mjini Windhoek, mji mkuu wa Namibia ambako alilazwa hospitalini baada ya kugunduliwa kwa seli za saratani wakati wa kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu, kulingana na ofisi ya rais.

"Ni kwa huzuni na masikitiko makubwa tunataarifu kwamba mpendwa wetu Dk. Hage G. Geingob, Rais wa Jamhuri ya Namibia, amefariki leo," imeandikwa taarifa iliyowekwa kwenye mtandao wa kijamii wa X, iliyotiwa saini na kaimu Mkuu mpya wa jeshi, Nangolo Mbumba, ambaye ni makamu wa rais.

Hage Geingob ambaye alichaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2014, alichaguliwa tena mnamo mwaka 2019 kama rais wa Namibia, nchi ya jangwani inayopatikana kusini mwa Afrika, moja ya nchi za mwisho barani iliyepata uhuru mnamo mwaka 1990.

Hage Geingob alikuwa amezungukwa na mke wake na watoto wake wakati wa kifo chake katika Hospitali ya Lady Pohamba katika mji mkuu, taarifa imesema.

Mwezi uliopita, ofisi ya rais ilitangaza kwamba uchunguzi wa mara kwa mara wa matibabu umegundua uwepo wa "seli za saratani" kwa mkuu wa nchi na kutaja kwamba atafuata "matibabu yanayofaa", huku akienelea na majukumu yake.

Hage Geingob alikuwa tayari amepata matatizo ya kiafya, ikiwa ni pamoja na kabla ya kuingia madarakani. Mnamo mwaka 2013, alifanyiwa upasuaji wa ubongo. Mwaka jana, alifanyiwa upasuaji wa aorta nchini Afrika Kusini, nchi jirani ya Namibia.

"Taifa la Namibia limepoteza mtumishi mashuhuri wa watu, kinara wa mapambano ya ukombozi, mbunifu mkuu wa Katiba yetu na nguzo ya nyumba yetu ya Namibia," Nangolo Mbumba amesema.

"Kwa wakati huu wa huzuni kubwa, natoa wito kwa taifa kuwa watulivu na kujikusanya," ameongeza.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.