Pata taarifa kuu

Sudan: Papa Francis ametoa wito wa usitishwaji wa mapigano

Nairobi – Kiongozi wa kanisa katoliki duniani, Papa Francis, ametoa wito kwa makundi yanayopigana nchini Sudan kusitisha vita iliyodumua kwa miezi 10 hivi sasa, ambapo imesababisha mamilioni ya watu kuhama makazi yao na kuzua hofu ya baa la njaa.

Aidha Papa Francis, amezungumzia mizozo inayoendelea nchini Msumbiji, Ukraine, Israel na Palestina
Aidha Papa Francis, amezungumzia mizozo inayoendelea nchini Msumbiji, Ukraine, Israel na Palestina AP - Andrew Medichini
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza katika ibada ya kila Jumapili mjini Vatican, Papa Francis, aliziomba pande hasimu kukomesha mapigano, aliyosema yamesababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu na maafa kwa raia wasio na hatia.

Kiongozi huyo aliongeza kuwa, ni imani yake kuwa viongozi wanaopigana watasikia mwito wake na kurejea katika meza ya mazungumzo ili kupata suluhu ya kudumu.

Mapigano kati ya makundi mawili ya kijeshi yamesababisha mamia ya raia wa Sudan kutoroka makazi yao
Mapigano kati ya makundi mawili ya kijeshi yamesababisha mamia ya raia wa Sudan kutoroka makazi yao AFP - -

Mwito wake unakuja wakati huu, Juhudi za kidiplomasia zikiwa zimeshindwa kumaliza vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini humo kati ya jeshi la Serikali na wapiganaji wa RSF.

Aidha Papa Francis, amezungumzia mizozo inayoendelea nchini Msumbiji, Ukraine, Israel na Palestina, akiwataka viongozi wa dunia kuwajibika kikamilifu katika kutafuta suluhu ya yanayoendelea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.