Pata taarifa kuu

Uchaguzi wa Urais nchini Senegal: Rais Sall ashutumiwa kwa kuchelewesha uchaguzi

Wagombea 15 wa urais nchini Senegal wamemshutumu mkuu wa nchi Macky Sall kwa "nia mbaya", na kutangaza hatua za kuhakikisha kuwa tarehe ya uchaguzi, iliyoahirishwa hadi tarehe ambayo bado haijaamuliwa, inatangazwa haraka.

"Kila kitu kinaendana na mtindo wa nia mbaya ya Rais Macky Sall," wanasikitika wapinzani wa rais wa Senegal.
"Kila kitu kinaendana na mtindo wa nia mbaya ya Rais Macky Sall," wanasikitika wapinzani wa rais wa Senegal. AFP - JOHN WESSELS
Matangazo ya kibiashara

Vuguvugu la wananchi "Aar Sunu Election" ("Hebu tulinde uchaguzi wetu") kwa upande wake limetangaza maandamano mapya siku ya Jumamosi. Vuguvugu hilo linataka uchaguzi huo ufanyike kabla ya Aprili 2, tarehe rasmi ya mwisho ya muhula wa Rais Sall. Kulingana na makadirio yake, uchaguzi huo, uliopangwa kufanyika Februari 25, lazima ufanyike Machi 3 hivi karibuni.

"Kuchelewa kusikoweza kuelezeka kumeonekana. Hakuna kilichofanyika" licha ya maendeleo ya wiki iliyopita, wanasema wagombea 15 katika taarifa ya pamoja iliyochapishwa siku ua Jumanne jioni. "Kila kitu hufanya kazi kwa mtindo wa nia mbaya ya Rais Macky Sall," wanasema.

Miongoni mwa viongozi hao 15 waliotia saini ni pamoja na meya wa zamani wa Dakar Khalifa Sall na, kupitia mwakilishi wake, Bassirou Diomaye Diakhar Faye, aliwasilisha kama mgombea badala ya mpinzani wa Ousmane Sonko. Mabwana Faye na Sonko wanazuliwa kwa sasa.

Senegal inapitia mzozo wa kisiasa ambao haujashuhudia kwa miongo kadhaa baada ya uamuzi wa mapema Februari wa Rais Sall na Bunge la Kitaifa kuahirisha uchaguzi wa rais. Uahirisho huu, uliolaaniwa kama "mapinduzi ya kikatiba" na upinzani, ulichochea maandamano ambayo yalisababisha vifo vya watu watatu. Wiki iliyopita, Baraza la Katiba lilibatilisha kuahirishwa kwa uchaguzi wa uraisi na kubakishwa kwa Rais Sall katika wadhifa wake hadi kuteuliwa kwa mrithi wake.

Baraza lilibaini kutowezekana kwa kudumisha uchaguzi wa rais mnamo Februari 25 na likaomba mamlaka kupanga "haraka iwezekanavyo" tareh ya uchaguzi. Rais Sall alisema mnamo Ijumaa nia yake ya kuheshimu uamuzi wa Baraza na kutekeleza "bila kuchelewesha mashauriano muhimu" ya kuandaa uchagzi.

Wasenegal sasa wanasubiri kujua tarehe mpya. Hakuna kilichofichuliwa hadharani kuhusu mijadala ambayo Rais Sall ataongoza. Wagombea hao 15 wanasema mchakato wa uchaguzi ulifaa kuanza tena. Wanamshutumu Rais Sall kwa kukataa kushika dhamira yake ya kuandaa uchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.